Mtandao wa kimataifa Alkafeel wafungua ukurasa mpya uitwao (Barua kwa Abulfadhil Abbasi –a.s-)…

Maoni katika picha
Pindi yanapokua masafa baina yako na yule unaye mpenda ni marefu sana.. na pindi unapoishi ukiwa na ndoto njema ya kufikisha unacho fikiria kwake.. na pindi unapokosa uwezo halafu akatokea wakukusaidia kubeba upendo wako na ujumbe wako na kumfikishia mpenzi wako.. bila shaka fursa hiyo hutokea mara chache kwa wapenzi..

Lakini jopo la watalamu wanaofanya kazi katika mtandao wa kimataifa Alkafeel wamechukua jukumu la kubeba barua za wapenzi zilizo andikwa kwa wino wa matumaini na kuzipeleka kwa mlango wa haja Abulfadhil Abbasi (a.s), hakika hii ni fursa ya pekee iliyokua ndoto ya wapenzi na wafuasi (wa watu wa nyumba ya mtume –a.s-) jopo hili limeifanya kua kweli ndoto zao, kwa kufungua ukurasa mpya uitwao (Barua kwa kaburi la Abulfadhil Abbasi –a.s-), huduma hii imeingizwa katika orodha ya huduma zilizo ongezwa kwenye mtandao.

Ukurasa huu kwa mujibu wa maelezo ya Ustadh Haidari Mamitha mkuu wa idara ya intaneti ambayo mtandao wa Alkafeel unatokana na idara hiyo, amesema kua: “Ukurasa huu umesanifiwa na kupangiliwa na wataalamu wa idara, unamambo mengi ya kitalamu, hii inaonyesha maendeleo yaliyopo katika sekta hii, pamoja na kuzingatia wepesi katika utumiaji na usiri katika utumaji wa barua hizo, kaandaliwa mtaalamu maalumu kwa ajili ya kazi hiyo”.

Akaongeza kusema kua: “Ukurasa huu upo pamoja na kurasa zingine za mtandao, mtu yeyote baada ya kuingia katika mtandao wa Alkafeel anaweza kuingia katika ukurasa huu na kutuma barua kama ilivyo katika mitandao mingine, na wala ukurasa huu haupo katika mtandao wa kiarabu peke yake, barua hizo zitatolewa (printiwa) na kuwekwa katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Mamitha akaendelea kubainisha kua: “Ukurasa huu una vitu vingi na miongoni mwa vitu hivyo ni:




    • - Imetengenezwa njia ya utafutaji nyepesi kuitumia.




    • - Kila mtumiaji anaweza kufungua Acount maalum atakayo tumia kutuma barua au anaweza kutuma hata bila Acount.




    • - Mtumiaji anaweza kutuma zaidi ya barua moja.




    • - Ukurasa unafanya kazi kwa lugha zote zilizopo katika mtandao wa Alkafeel.




    • - Mtumiaji atatumiwa alama katika anuani ya barua pepe yake ya kukubaliwa kwa barua na kuprintiwa sambamba na kuonekana alama hiyo katika sehemu aliyotumia kujisajili.




    • - Ukurasa unakubali kufunguka na kutumika katika aina zote za simu (smart phone) na (tablet) pamoja na kompyuta, ilitumiwa program ya (Ajax) katika kupangiliwa kwake.




    • - Kutafuta ni rahisi, unatumia alama yenye herufi na namba 8.




    • - Imezingatiwa mipaka inayo kubalika kwa watumishi wa intaneti katika utendaji wa ukurasa huu.




Ukitaka kuangalia zaidi vipengele hivi na vinginevyo unaweza kuingia katika mtandao ufuatao:https://alkafeel.net/message/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: