Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya juhudi ya kuendeleza teknolojia katika mitambo ya elektronok inayo fanya kazi katika maeneo muhimu, kupitia fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhudhuria katika maonyesho ya kitalamu yanayo fanywa ndani na nje ya Iraq, na miongoni mwa maonyosho muhimu ni yale yaliyofanywa Dubai ya teknolojia ya kiusalama ya hali ya juu.
Atabatu Abbasiyya tukufu ilituma ujumbe wa jopo la wahandisi katika maonyesho hayo, akiwemo Muhandisi Farasi Abbasi Hamza ambaye ametuambia kua: “Lengo kuu la kuhudhuria maonyesho haya ni kuangalia teknolojia mpya, na kutambua maendeleo yaliyo patikana katika mitambo ya ulinzi na kamera, na kuilinganisha na ile iliyopo katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuangalia namna ya kuiendeleza na kuifanya kua na uwezo mkubwa, jambo ambalo ni kupiga hatua kwenda mbele na kupambana na changamito za kiusalama za sasa zinazo weza kuukumba mji wa Karbala hususan Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya”.
Akaongeza kusema kua: “Uwepo wetu katika maonyesho haya na matembezi tuliyo fanya katika meza mbalimbali za maonyesho, tumeona vifaa na mitambo ambayo ni muhimu kwa vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kama vile kitengo cha kulinda nidham, magodauni, mitambo pamoja na utaratibu maalumu uliopo katika idara ya mawasiliano”.
Muhandisi Farasi akabainisha kua: “Tumejadiliana kuhudu utendaji wa mtambo wa kuhariri video wa idara ya mawasiliano, tulipo kutana na mkuu wa shirika linalo tengeneza mitambo hiyo, na tumeandika maoni yote na kuyatuma kwenye shirika la (Iomniscient) kitengo cha uchunguzi na uboreshaji cha shirika hilo kwa ajili ya kuutengeneza na kutupa uzowefu wao”.
Akaendelea kusema kua: “Hali kadhalika tulikutana na mwakilishi wa shirika lililo tengeneza mtambo wa kuhesabu (watu) mazuwaru, kwa ajili ya kuweka mpango kabambe wa kuboresha uwezo wa mtambo huo na kuweka vitu vingine vitakavyo saidia kuongeza uwezo wa mtambo hususan katika kuhesabu (watu) mazuwaru wakati wa kipindi cha maombolezo na matembezi ya tuwaleji, amma kuhusu mtambo wa ulinzi, ambao ni miongoni mwa mitambo ya kisasa zaidi iliyopo Iraq, tayali nao umewekewa mkakati wa utendaji wake, baada ya kukutana na wawakilishi mbalimbali kutoka katika mashirika ya kimataifa kwa ajili ya kuuboresha na kuufanya uwe wa kisasa zaidi kushinda ulivyo sasa na kuufanya uweze kubeba kamera nyingi zaidi ili kupanua wigo wa kazi yake katika siku za usoni”.
Akaashiria kua: “Pia tumekagua mafanikio ya mashirika yanayo tengeneza kamera zenye teknolojia ya kisasa, pamoja na mitombo mingine inayo husu baadhi ya vitengo vya Ataba tukufu, kama vile mtambo unao hamishika wa kukagua mabeji na kamera za mkononi, na mtambo wa kukagua vilipuzi (mabomu), na mingineyo miongoni mwa mitambo inayo weza kutumika katika vitengo mbalimbali vya Ataba na ikasaidia kuboresha huduma kwa mazuwaru kipindi cha ziara zao”,
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inamiliki mtambo wa ulinzi wa kisasa miongoni mwa mitambo bora zaidi duniani, mtambo huo unahitaji maboresho endelevu kwa ajili ya kuongeza ubora wake na kuhakikisha unafanya kazi muda wote kwa ajili ya kulinda usalama wa mazuwaru watukufu.