Kwa ushiriki wa wanafunzi (45): Umeanza mchujo wa kwanza wa shindano la kitaifa la fani ya kukhutubu la wanafunzi wa shule za sekondari…

Maoni katika picha
Mwaka wa tatu mfululizo chini ya kauli mbiu isemayo: (Kwa mwito wa Twafu tumeitikia na kwa utukufu wa fatwa tumeshinda), asubuhi ya Alkhamisi (12 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (01 Machi 2018m) umeanza mchujo wa kwanza wa shindano la fani ya kukhutubu kwa wanafunzi wa shule za sekondari, ambalo litafanyika kufuatia ushindi walio pata jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi dhidi ya magaidi wa Daesh.

Shindano hili hufanywa kila mwaka na idara ya harakati za shule zilizo chini ya idara ya mahusiano na vyuo vikuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, katika mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo, na kwa kushirikiana na ofisi za malezi katika mikoa ya kati na kusini, awamu hii ya mashindano wanashiriki wanafunzi (45) kutoka mikoa kumi, ambayo ni: (Bagdad, Karbala tukufu, Najafu Ashrafu, Alqadisiyya, Albasra, Waasit, Dhiqaari, Baabil, Muthanna na Misaani), kutakua na vikao viwili, kikao cha wanza kitafanyika asubuhi na kingine jioni, vikihusisha wale watakao shiriki mwishoni mwa shindano litakalo anza rasmi asubuni ya kesho InshaAllah.

Kikao cha uchujaji kimefanyika katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) kimefunguliwa kwa Qur’an tukufu, na kimehudhuriwa na wawakilishi wa ofisi za malezi pamoja na washiriki na familia zao, kisha ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya, halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq.

Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Shekh Muhammad Kuraitwi kutoka katika kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa aliyo sema ni: “Muhanga wa Imamu Hussein (a.s) umekua ni mfano mkubwa wa kujitolea, jihadi na kuonyesha msimamo, pamoja na juhudi zote zilizo fanywa za kutaka kuzima nuru ya muhanga huo bado umeendelea kung’ara na kua mfano safi”.

Akaongeza kusema kua: “Zimetukuka roho zinazo beba msimamo wa bwana wa mashahidi (a.s) kutokana na fatwa tukufu iliyo tolewa na Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani ambayo ilikua tiba ya majeraha ya Iraq, na mwiba katika jicho la dhalimu, wananchi wa Iraq wameithibitishia dunia na historia kwa kufuata kwao nyayo za jeshi la bwana wa mashahidi (a.s), na wamethibitisha kushikamana kwao na maelekezo mema ya Marjaiyya, wakajitokeza vijana shupavu wakiitikia mwito wa fatwa tukufu iliyo twaharisha ardhi kutokana na magenge ya kigaidi”.

Akaashiria kua: “Tabaka zote za jamii zilijitolea na kusimama pamoja na wapiganaji wa vikosi vyote kuanzia jeshi la serikali na Hashdi watukufu (wapiganaji wa kujitolea) waliwapa msaada wa hali na mali, jambo hilo ni miongoni mwa sababu kubwa za kupata ushindi, hususan kazi kubwa ya pekee imefanywa na ndugu zetu walimu na wanafunzi kwa kufanya makongamano, nadwa na kuandika mada mbalimbali zilizo bainisha utukufu wa vita hiyo ya kihistoria, na shindano hili ni moja kati ya ushahidi wa wazi wa nafasi kubwa waliyo nayo katika swala hili”.

Baada ya hapo wanafunzi wanaoshiriki walianza kuwasilisha khutuba zao kwa kupanda katika jukwaa la ukumbi, uwasilishaji wao unapimwa kwa vigezo maalum vilivyo wekwa na kamati inayo ongozwa na Dokta Said Hamiid Kaadhim na Dokta Alaa Swaaleh Abiid (mjumbe) na Ustadh Saamir Hassan Mansuur (mjumbe).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: