Muendelezo wa maandalizi ya kongamano la (Ruhu Nubuwwah), na kamati ya maandalizi yasisitiza kua litapendeza sawa na makongamano ya kimataifa…

Sehemu ya kongamano
Kamati ya maandalizi ya kongamano la (Ruhu Nubuwwah) pamoja na kamati ndogo ndogo zinazo tokana na kamati hiyo, zinaendelea na maandalizi ya awamu ya pili ya program ya kiutamaduni inayo fanywa kwa mwaka wa pili mfululizo na idara za shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatuma (a.s) ni mwendelezo wa utume na uwa la peponi) kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu tukufu ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na kuangazia utukufu wake kwa kutumia vitu mbalimbali vitakavyo fanyika katika kongamano.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyo tolewa na mkuu wa kamati ya maandalizi ya kongamano Ustadhat Bushra Jabbaar kwenye mtandao wa Alkafeel, ambapo amebainisha kua: “Hivi sasa tupo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kongamano hili, litakalo anza tarehe ishirini ya mwezi wa Jamadal-Thani, tayali umesha teuliwa ukumbi wa kongamano, ambao utakua ukumbi mkuu wa kituo cha Swidiqatu Kubra (a.s), tayali imesha andaliwa ratiba na kupangiliwa mambo yote yatakayo fanyika, pamoja na kuandaa makazi ya wageni na kutuma mialiko kwa watafiti wa kisekula na kihauza kwa ajili ya kuhudhuria na kushiriki, sambamba na kutuma mialiko kwa vyombo vya habari kwa ajili ya kuja kuripoti tukio hili muhimu na kubwa linalo tokana na harakati za wanawake wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akabainisha kua: “Kuna juhudi kubwa sana zinazo fanywa na wakina dada wa kitengo cha Zainabiyya na idara ya ofisi ya wanawake pamoja na idara ya redio ya shule za Ameed na Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya kitengo cha maarifa, sambamba na idara ya kituo cha Swadiqa na watumishi wake kwa ajili ya kuhakikisha kongamano hili linakua na muonekano bora zaidi”.

Ustadhat Bushra akasisitiza kua: “Kuna kila dalili zinazo ashiria kua kongamano hili litafana zaidi ya kongamano lililo pita, kutokana na kuwepo kwa ratiba mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushiriki wa kimataifa, hadi sasa idadi ya nchi zitakazo shiriki ni zaidi ya kumi ukiongeza na mwenyezi wao Iraq, wakati mwaka jana zilishiriki nchi sita tu, hali kadhalika mada zitawasilishwa kisasa na zinaujumbe muhimu unao hitajika na maktaba za wanawake kwa ajili ya tafiti mbalimbali”.

Fahamu kua tayali zimesha tangazwa mada zilizo faulu kuingia katika shindano la kitafiti litakalo fanyika katika kongamano hili, kwa kuangalia hilo bonyeza hapa, https://alkafeel.net/news/index?id=6482.

Kumbuka kua lengo la kongamano hili ni kubainisha nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) katika kila sekta, na kutoa pazia kuhusu nafasi yake katika elimu kupitia mada zinazo wasilishwa na kuonyesha nafasi yeke kielimu, na kuzizawadia maktaba maalumaat kuhusu mtu huyu mtukufu na nafasi yake kielimu na kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: