Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wananadi: Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako ewe Abulfadhil Abbasi katika kumbukumbu ya kufariki mama yako Ummul Banina (a.s)…

Maoni katika picha
Wengi wanakuja duniani na wanaondoka kama walivyo kuja hawaachi ispokua majina tu, tofauti na watu ambao umebaki utajo wao unagonga vichwa vya historia katika zama zote, miongoni mwao ni watu wa nyumba ya Utume na mashukio ya wahyi ambao hawafananishwi na yeyote wala hakuna kiumbe anaye fikia hadhi yao, miongoni mwa watu watukufu walio lelewa na wakaishi katika nyumba hii tukufu ambayo malaika wa mbinguni walikua wanajifaharisha kwa kuwatumikia ni bibi Fatuma bint Hizaam anaye julikana kwa jina la Ummul Banina ambae ni mama wa Abbasi (a.s).

Kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kifo chake (a.s) ambacho kilitokea siku kama ya kesho Ijumaa (13 Jamadal-Thani), watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wametoka katika maukibu (matembezi) ya kuomboleza kwa ajili ya kutoa taazia kwa mnusuruji wa ndugu yake Imamu Hussein (a.s) na kamanda wa jeshi lake na mlezi wa familia yake Abulfadhil Abbasi (a.s), huku hali ya mazingira yao ikisema: Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako ewe bwana wangu ewe Abulfadhil Abbasi kwa msiba huu.

Aina hii ya kuomboleza ndio iliyo zoweleka na watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika kuhuisha matukio kama haya, imekua ada katika kuhuisha kumbukumbu za vifo vya Maimamu watakasifu (a.s), hutoka maukibu (matembezi) ya kuomboleza kuanzia katika Atabatu Abbasiyya tukufu hadi katika ukumbi wa haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), lakini katika kumbukumbu ya kifo cha Ummul Banina (a.s) hua tofauti, watumishi wa Imamu Hussein (a.s) hufanya matembezi na kupokewa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ukumbi wa haram yake takatifu.

Kisha hufanywa majlisi ya pamoja ya kuomboleza, na husomwa kaswida na mashairi yanayo elezea hadhi na utukufu wa mama huyu kihistoria, aliye tumia umri wake wote katika kuwalea Hassan na Hussein (a.s) mabwana wa vijana wa peponi, aliwatanguliza katika kila jambo kuliko watoto wake mwenyewe, historia haija ripoti mwanamke aliye wapenda mno watoto wa mumewe kuliko watoto wake na akajitolea watoto wake wafe kwa ajili ya kulinda watoto wa mumewe zaidi ya mama huyu mtukufu, yeye alijua kufanya hivyo ni wajibu kidini, kwani wao ni zawadi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), Ummul Banina alitambua hilo akasimama imara kuwatumikia.

Kumbuka kua Ummul Banina (a.s) baada ya kumtumikia bwana wa mawasii na watoto wake maimamu wawili Hassan na Hussein (Hassanain) na Aqilah bani Hashim Zainabu Kubra (a.s), umri wake mtukufu aliutumia kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu, na aliishi na huzuni kipindi kirefu kutokana na kuwakosa mawalii wa Mwenyezi Mungu mtukufu, na matukio ya kutisha aliyo shuhudia, kuanzia kuuawa kwa Imamu Ali bun Abu Twalib kwa kupigwa panga katika mihrabu yake, na kifo cha mwanae Imamu Hassan (a.s), na kuuawa kwa watoto wake wanne ndani ya saa moja, waliokua wakilinda heshima ya mpenzi wa Mwenyezi Mungu na mjukuu wa mtume wake Imamu Hussein (a.s), baada ya kushuhudia yoto hayo alifariki mwezi kumi na tatu Jamadal-Thani mwaka wa 64 hijiriyya, akaenda katika rehma za Mola wake mtukufu na akazikwa katika makaburi ya Baqii karibu na kaburi la Ibrahim, Zainabu, Ummu Kulthum, Abdallah, Qassim na wengineo miongoni mwa maswahaba na mashahidi, kaburi lake lilibomolewa na manawaasib pamoja na makaburi ya maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Amani iwe juu ya mwanamke mtukufu na mtakasifu, mtekelezaji mwenye ikhlasi, aliye fata nyayo za mbora wa wanawake wa ulimwenguni Fatuma Zaharaa (a.s) kisheria na kimwenendo, pongezi kubwa ziwe juu yake na juu ya kila atakaye fuata mwenendo wao miongoni mwa wanawake wema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: