Baada ya siku mbili za kusajili khutuba: pazia limefunguliwa la mashindano ya kitaifa katika fani ya kukhutubu kwa wanafunzi wa shule za sekondari…

Maoni katika picha
Baada ya siku mbili za kupitia khutuba zilizo sajiliwa za wanafunzi washiriki (45) kutoka katika mikoa ya kati na kusini, pazia limefunguliwa asubuhi ya Ijumaa ya leo (13 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (2 Machi 2018m), pazia la mashindano ya kitaifa ya awamu ya tatu katika fani ya kukhutubu kwa wanafunzi wa shule za sekondari, yanayo simamiwa na idara ya harakati za shule zilizo chini ya idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na Atabatu Abbasiyya tukufu ikiwa ni miongoni mwa mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo chini ya kauli mbiu isemayo: (Tumeitikia wito wa Twafu na tumeshinda kutokana na fatwa) na kwa kushirikiana na ofisi za malezi katika mikoa ya (Bagdad, Karbala tukufu, Najafu Ashrafu, Qadisiyya, Basra, Waasit, Dhiqaar, Baabil, Muthanna na Misaan).

Hafla ya kufunga tukio hili imefanywa katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), baada ya kusomwa Qur’an ya ufunguzi kulikua na ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Shekh Swalahu Karbalai rais wa kitengo cha dini, alitoa pongezi nyingi kwa wanafunzi walio fanya vizuri na kupata nafasi za kwanza, akawataka wajiendeleze zaidi na kukuza vipaji vyao.

Akaongeza kusema kua: “Hakika utoanji wa khutuba ni muhimu, Qur’an tukufu imesisitiza sana nafasi ya khutuba katika uhai, khutuba ni hekima, mapinduzi, uhai na ni rehma, miongoni mwa mambo muhimu sana katika masharti ya khutuba, unatakiwa ukiamini unacho khutubia”.

Karbalai akabainisha kua: “Mradi wa mashindano ni mradi muhimu wa kitamaduni, yapasa kuuendeleza na kuufanya kila mwaka, kutokana na umuhimu wake wa kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto vya kutoa khutuba”, vilevile akasifu nafasi za ofisi zinazo shiriki kwa kusaidiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, na mchango wao katika kuhakikisha shindano linafaulu na linakua na muonekano bora.

Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa vituo vya malezi vinavyo shiriki ulio wasilishwa na Ustadh Hassan Shawili mkuu wa harakati za shule katika wizara ya malezi, akatoa shukrani kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na akapongeza tukio hili linalo onyesha uwajibikaji wao katika kukuza vipaji vya wanafunzi kwenye sekta ya kutoa khutuba, pia akasisitiza umuhimu wa kudumisha ushirikiano kati ya wizara na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuwajenga wanafunzi kinafsi na kiakili.

Baada ya hapo wanafunzi watano walio tangazwa na kamati ya majaji kua washindi wakapanda katika jukwaa na wakazungumza kuhusu taifa lao la Iraq.

Halafu kamati ya majaji inayo ongozwa na Dokta Saidi Hamidi Kaadhim na Dokta Alaa Swaaleh Abiid (mjumbe) na Ustadh Saamir Hassan Mansuur (mjumbe) walibainisha kua, walifuata kanuni na vigezo maalum katika kuzipima khutuba, tunakuletea majina ya washindi watano wa shindano hili:

Nafasi ya tano: Mwanafunzi Abbasi Ghazi Abbasi kutoka katika ofisi ya malezi za Baabil.

Nafasi ya nne: Mwanafunzi Muhammad Jafari Ali Jafari kutoka katika ofisi ya malezi za Najafu Ashrafu.

Nafasi ya tatu: Mwanafunzi Muntadhir Abdul-Adhim Faahim kutoka katika ofisi ya malezi za Qadisiyya.

Nafasi ya pili: Mwanafunzi Muhammad Farasi Twaha kutoka katika ofisi ya malezi za Misaan.

Nafasi ya kwanza: Mwanafunzi Haidari Farasi Abdul-Abbasi kutoka katika ofisi ya malezi za Raswafatul-Ula (Bagdad).

Mwisho kabisa wa shindano hili ulikua ni ugawaji wa zawadi kwa washindi, sambamba na kugawa vyeti vya ushiriki kwa wanafunzi wote walio shiriki pamoja na ofisi za malezi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: