Sayyid Sistani: Pindi ninapo wakumbuka mashahidi wa Hashdi Sha’abi nakumbuka kujitolea kwa maswahaba wa Imamu Hussein (a.s) kwenda Madina…

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesisitiza kua ni jambo la kawaida kupotoshwa historia, kwani vita na ushindi huletwa na makamanda shupavu na hunufaisha waoga, hivi ndivyo historia inavyo tufundisha, iwapo hayata andikwa mambo yaliyo jiri kuanzia pale ilipo tolewa fatwa tukufi hadi leo, hata kama ukiwa uandishi sio mzuri, kwa sababu baada ya miaka ya matatizo na mitihani mtasahaulika, na tutakapo hitaji ushahidi wa kupigana kwenu ili tuonyeshe kwa wasomaji hautapatikana.

Aliyasema hayo katika kikao chake na wapiganaji wa kikosi cha Imamu Ali (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, akaongeza kusema kua: “Imamu Hussein (a.s) alikua na kundi dogo miongoni mwa maswahaba zake walio kua wakiwakilisha kundi kubwa, kisha likaongezeka kidogo kidogo hadi lio limeenea dunia nzima, tumesikia kutoka kwa Sayyid Sistani kwamba, alikua anapo mtaja au anapo mtembelea ndugu yetu wa Hashdi Sha’abi, alikua anahisi sawasawa na kuwakumbuka maswahaba wa Imamu Hussein (a.s) walipo kua wakimiminika kwenda Madina, Tumesikia kutoka kwake moja kwa moja na tukamuomba aandike kitu kwa mkono wake kuhusu mashahidi, kwa sababu tulikusudia kufanya jambo litakalo kua na ushahidi zaidi na kusambaza kwa familia za mashahidi, tukatarajia aandike maelezo kuhusu mashahidi, hakika aliandika kwa mkono wake mtukufu maneno ambayo yamekua mashuhuri hivi sasa.

Mnapaswa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha kuacha starehe za dunia na kuingia katika uwanja wa mapigano, kila mmoja katika nyie anapo ingia vitani anatarajia kupata shahada, lakini Mwenyezi Mungu mtukufu amekubakisheni ili awawezeshe kufanya ibada zingine, mwanadamu anaye fanya biashara na Mwenyezi Mungu bila shaka Mwenyezi Mungu atamlipa zaidi, Mwenyezi Mungu sio bahili atamkirimu sana, mnatakiwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, kuna watu wa umri wenu wanafanya mambo mengine hawajaingia katika neema hii mliyo ingia nyie hongereni sana kwa hadhi tukufu mliyo nayo”.

Sayyid Swafi akaendelea kusema kua: “Kuna nukta naisisitiza ambayo ni muhimu sana, leo mnashuhudia yanayo fanyika kwa sababu mpo wakati wa tukio, lakini baada ya miaka (50) au zaidi kuthibitisha yaliyo tokea leo kutahitajia ushahidi tofauti na ushahidi unaohitajika leo, leo umevaa nguo za kijeshi, unashiriki katika uwanja wa vita, unashuhudia yanayo fanyika, baada ya kupita muda mrefu vielelezo hivi vitapotea havita bakia milele, nini mbadala wake? Mbadala wake ni kuandika na kutunza kumbukumbu ya kila kinacho fanyika”.

Akaongeza kusema kua: “Hivi sasa inawapasa kuandika kila mnacho kifanya kwa sababu baada ya miaka ya mateso na mitihani ya vita mliyo pigana kwa juhudi kubwa, tutahitaji ushahidi wa kuthibitisha mchango wenu, historia ina matukio mengi ambayo hayakutufikia kwa sura sahihi, kwa sababu yaliingiliwa na waongo pamoja na wapotoshaji wa historia, yakaingia katika ndimi za waandishi waongo na yameendelea kupotoshwa hadi leo”.

Akabainisha kua: “Sisi tunaandika mausua (kitabu) kinacho elezea kwa kina mambo haya kitakacho kua na juzuu (25), tumesha anza kazi hiyo na baadhi ya juzuu zake zimesha kamilika, lakini tunahitaji msaada wenu na wa marafiki zenu kutokana na matukio mliyo yaona katika viwanja vya vita ili tusiandike mambo nusu, pamoja na kutunza kumbukumbu hizi kuna jambo lingine, vizazi vya kesho baada ya kupita miaka mingi vitaulizana, walifanya nini baba zetu pale Iraq ilipo vamiwa na magaidi wa Daesh, ni vizuri mmoja kati yao ainue kichwa na kusema baba yangu au babu yangu alifanya hivi na hivi, kama ilivyo leo tunajifaharisha na baadhi ya familia kwa yaliyo fanywa na mababu zao, wanasema: baba yangu au babu yangu alichangia katika kuikomboa Iraq kutoka mikononi mwa Daesh na aliitikia mwito wa Marjaiyya na akashiriki katika vita nyingi sana, hii hapa historia yake inabainisha aliyo fanya yeye pamoja na rafiki zake kwa ajili ya kulinda taifa”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Watu wa Iraq tuna mambo mengi mazuri lakini tuna kasoro moja ya kutotunza matukio yetu, hivyo mtu yeyote anaweza kuja na akadai kua mimi nilifanya hiki na hatutaweza kumpinga kwa sababu hatuna ushahidi, tukio ni kweli lilitokea lakini halina ushahidi, kutunza ushahidi ni muhimu sana hata ukiwa wa maneno (kurekodi sauti) kwa kiasi ambacho wajukuu zako wataisikiliza na kujifaharisha kwa yale uliyo ifanyia Iraq kipindi hiki”.

Baada ya hapo kamanda wa kikosi cha Imamu Ali (a.s) Shekh Karim Khaqani akaelezea maeneo muhimu wanayo yadhibiti na vita waliyo pigana, pamoja na idadi ya wapiganaji wake na vifaa vya kijeshi walivyo navyo, kisha Sayyid Ahmadi Swafi akakabidhi bendera ya kikosi na baadhi ya zawadi zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: