Mawakibu za kuomboleza kutoka ndani na nje ya Karbala katika siku kama ya leo, mwezi kumi na tatu Jamadal-Thani zimezowea kumiminika katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kumpa pole kutokana na kifo cha mama yake bibi mtukufu na mtakasifu Ummul Banina (a.s), kwani yeye ndiye anaye stahiki zaidi kupewa pole katika msiba huu, mawakibu na mazuwaru wamezowea kuomboleza kwa mtindo huo, mawakibu zilianza kumiminika katika haram yake tukufu toka jana hadi leo kwa kufuata utaratibu ulio pangwa na kitengo cha mawakibu na vikundhi vya Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Mawakibu (misafara) ya kuomboleza zilipitia barabara ya kibla ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hadi mbele ya kaburi lake tukufu na kumpa pole huku wakitaja msimamo imara alio onyesha siku ya Ashura na kabla ya siku hiyo na baada yake, alipo jitolea nasfi yake kwa ajili ya kumlinda ndugu yake Imamu Hussein (a.s), walipaza sauti na kutokwa machozi kutokana na msiba huu ulio ifika nyumba ya Ma-Alawi katika mwaka wa 64 hijiriyya, huku mazingira yao yanasema: Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako ewe mwenye msiba ewe Abulfadhil Abbasi kwa tukio hili chungu.. kisha baada ya hapo maukibu (misafara) zinaelekea katika malalo ya Imamu Hussein (a.s), wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Rais wa kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu maadhimisho haya kua: “Katika kumbukumbu ya kifo cha Ummul Banina (a.s), mawakibu zinaanza kuwasili siku moja kabla ya tarehe rasmi ya kumbukumbu ya kifo hicho, ambayo ni mwezi kumi na tatu Jamadal-Thani na wanaendelea hadi baada ya siku hiyo, na kilele chake ni leo, ambapo malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) hupokea mawakibu nyingi zaidi kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, haya ni mazowea ya siku nyingi, watumishi wa kitengo chetu huratibu matembezi ya mawakibu (misafara), mawakibu zinaingilia mlango wa Kibla katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na baada ya kutoa pole kwake ukizingatia kua yeye ndio muhusika mkuu wa msiba huu, huelekea katika malalo ya Imamu Abu Abdillahi Hussein (a.s), wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, katika matembezi hayo pia hushiriki kundi kubwa la mazuwaru”.
Kumbuka kua Ummul Banina (a.s) baada ya kumtumikia bwana wa mawasii na watoto wake maimamu wawili Hassan na Hussein (Hassanain) na Aqilah bani Hashim Zainabu Kubra (a.s), umri wake mtukufu aliutumia kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu, na aliishi na huzuni kipindi kirefu kutokana na kuwakosa mawalii wa Mwenyezi Mungu mtukufu, na matukio ya kutisha aliyo shuhudia, kuanzia kuuawa kwa Imamu Ali bun Abu Twalib kwa kupigwa panga katika mihrabu yake, na kifo cha mwanae Imamu Hassan (a.s), na kuuawa kwa watoto wake wanne ndani ya saa moja, waliokua wakilinda heshima ya mpenzi wa Mwenyezi Mungu na mjukuu wa mtume wake Imamu Hussein (a.s), baada ya kushuhudia yoto hayo alifariki mwezi kumi na tatu Jamadal-Thani mwaka wa 64 hijiriyya, akaenda katika rehma za Mola wake mtukufu na akazikwa katika makaburi ya Baqii karibu na kaburi la Ibrahim, Zainabu, Ummu Kulthum, Abdallah, Qassim na wengineo miongoni mwa maswahaba na mashahidi, kaburi lake lilibomolewa na manawaasib pamoja na makaburi ya maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s).