Kukamilisha hatua za mwisho za maandalizi ya kongamano la awamu ya pili la Ruhu Nubuwwah…

Sehemu ya kongamano lililopita
Kamati ya maandalizi ya kongamano la Ruhu Nubuwwah imetangaza kukamilika maandalizi ya mwisho ya kongamano hilo linalo simamiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya tukufu yatakayo fanyika kwa awamu ya pili, wameongeza idadi ya vikao vya kujadili utekelezaji wa ratiba ya kongamano kwa ajili ya kuhakikisha linakua zuri na kukidhi viwango vya makongamano ya kimataifa, ili liendane na utukufu wa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) ambalo ni sehemu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na kuangalia mchango wake katika dini, jamii na familia, kongamano hili litafanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatuma (a.s) ni chemchem ya utume na tunda la peponi).

Rais wa kamati ya maandalizi ya kongamano hili Ustadhat Bushra Jabbaar Kinani ametuambia vipengele muhimu vya maandalizi ya mwisho kua: “Tumeweka vipengele vya mwisho mwisho katika maandalizi ya kongamano litakalo anza Alkhamisi ya wiki ijayo Inshallah, tumesha fanya vikao vingi na kamati tano ndogo ndogo zilizo teuliwa kuwakilisha idara saba za wanawake walio chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kiasi kikubwa kila kamati imekamilisha majukumu iliyo pewa. Kamati ya matangazo imeandaa mpango kamili utakao tekelezwa na redio Kafeel na idara ya ofisi ya wanawake na kuhakikisha upande wa matangazo upo sawa kwa kutumia vyombo vya habari mbalimbali, kama vile mahojiano ya kwenye redio, magazeti, mitandao ya kijamii, chanel za luninga (tv) pamoja na mawakala wa habari kwa ajili ya kuweka uwelewa mkubwa zaidi katika ulimwengu wa habari za wanawake”.

Akaongeza kusema kua: “Kamati ya elimu inayo ongozwa na Dokta Karimah Madani imeweka utaratibu maalum wa kupima mada zitakazo wasilishwa na kuhakikisha zitamuendeleza mwanamke wa Iraq na wakiarabu na kujenga vipaji vyao, pamoja na kuendeleza utamaduni, familia na jamii kutokana na faida za kielimu katika kujenga familia bora inayo nufaika na turathi na tamaduni za watu wa nyumba ya Mtume (a.s)”. kuhusu kamati ya mahusiano Kinani amebainisha kua: “Kamati hii imefanya kazi kubwa katika kipindi cha mwaka mzima, imewasiliana na waalikwa na kuwapa msaada ya kimkakati kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kuwakaribisha katika kongamano, ifahamike kua kuna wageni kutoka ndani na nje ya Iraq, na hao wa nje inahitajika juhudi zaidi”

Amma kuhusu sehemu litakapo fanyika kongamano ni makao makuu ya Swidiqah Twahirah (a.s), kwa mujibu wa maelezo ya Kinani: “Maandalizi yanaendelea vizuri ya kuandaa ukumbi wa ufunguzi wa kongamano pamoja na kumbi zingine zitakazo tumika katika program hii”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunacho tarajia tarehe ishirini Jamadal-Thani ni kufanikisha kongamano hili kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu, mafanikio hayo yatakua ndio matunda ya maandalizi haya na ushirikiano baina ya kamati zinazo fanya kazi kubwa kwa kusaidiana na kitengo cha Zainabiyya, idara ya redio, idara ya ofisi ya wanawake, shule za Ameed, Maahadi ya Qur’an tukufu bila kuisahau idara ya kituo cha Swidiqah Twahira”.

Kumbuka kua lengo la kufanya kongamano hili ni kubainisha nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) katika sekta zote, na kuondoa pazia kuhusu mchango wake wa kielimu kupitia mada zitakazo wasilishwa na kuonyesha nafasi yake katika elimu, na kutoa elimu kwa maktaba kuhusu utukufu wa mtu huyu na athari yake katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: