Kujali juhudi zao: Maahadi ya Qur’an tukufu inawapa zawadi Maustadhi walio shiriki katika mradi wa vituo vya Qur’an kwenye ziara ya Arubaini…

Maoni katika picha
Miongoni mwa miradi ya Qur’an iliyo simamiwa na Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), ni mradi wa vituo vya Qur’an, ulio tekelezwa na kamati kuu ya Qur’an tukufu inayo undwa na Ataba mbalimbali pamoja na Mazaru kwa kushirikiana na umoja wa vikundi vya Qur’an vya Iraq, ilitumia watalamu wake wa Qur’an kutoa huduma kwa mamilioni ya mazuwaru (watu) waliokua wakielekea kwa bwana wa mashahidi (a.s).

Kutokana na kuthamini juhudi hizo, Maahadi tukufu imeamua kuwapa zawadi Maustadhi walio shiriki katika mradi huo, kwa kufanya hafla asubuhi ya leo Juma Mosi (13 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (03 Machi 2018m) katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s).

Katika hafla hiyo mkuu wa Maahadi ya Qur’an Shekh Jawadi Nasrawi alisema kua: “Chini ya Atabatu Abbasiyya tukifu unafanyika ubobezi wa kila kitu katika sekta zote, za kielimu, kitamaduni na kiujenzi tena kwa kushuhudiwa na kila mtu, miongoni mwa harakati zao ni kuhusu Qur’an tukufu, na miongoni mwa harakati kubwa za Maahadi ya Qur’an ni mradi wa vituo vya Qur’an katika ziara ya Arubaini, unaolenga kusambaza utamaduni wa Qur’an na kuwafundisha mazuwaru usomaji sahihi wa Qur’an tukufu, hususan sura zinazo somwa katika swala, mradi huu ulikua na matunda mazuri”.

Akabainisha kua: “Wanufaika wa mradi huu walifika watu laki nne (400,000), jambo lililo tushajihisha zaidi na kutufanya tusiishie kutekeleza mradi huu katika ziara peke yake, bali tulifika hadi katika nyumba za watu na katika husseiniyyaat na misikitini, na ukatekelezwa kupitia matawi yetu katika miji mbalimbali, takwimu za mwaka (2017) zinaonyesha kulikua na zaidi ya vituo (150) katika barabara zinazo elekea Karbala, na Maustadhi walio shiriki kufundisha katika vituo hivyo ni zaidi ya (120), ambapo idadi ya wanufaika wao katika mwaka wa (2017) walifika laki moja na elfu themanini (180,000)”.

Pia kulikua na ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Shekh Aqiil Abedi kutoka katika kitengo cha dini, akabainisha umuhimu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na umuhimu wa kukitafakari, pamoja na umuhimu wa kukisoma vizuri na kufuata hukumu zake, na niwajibu wa kila muumini afanye juhudi hizi na ahakikishe anatumia vizuri kila fursa anayo ipata, miongoni mwa fursa hizo ni kipindi cha ziara ya Arubaini ambacho Maahadi ya Qur’an tukufu inasimamia mradi wa vituo vya Qur’an kwa ajili ya lengo hili, ndugu zetu watumishi wa kitengo hiki wamefanya juhudi kubwa sana katika swala hili, shukrani za dhati ziwaendee kwa juhudi zao na wandelee kufanya hivyo mwaka baada ya mwaka”.

Matawi ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika mikoa ya Iraq yaliyo tekeleza mradi huu walikua na ujumbe, na ukawasilishwa kwa niaba yao na mkuu wa tawi la Maahadi ya Qur’an tukufu katika wilaya ya Hindiyya, Sayyid Haadid Mar’abi, ambaye amesema kua: “Mradi wa vituo vya Qur’an ulio fanywa katika njia zinazo elekea Karbala, ni kwa ajili ya kutekeleza jukumu bora zaidi ambayo ni kutoa huduma kwa mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s) kwa kuwapokea, kuwashajihisha na kuwafundisha usomaji sahihi wa Qur’an tukufu, katika vituo vyetu vya Qur’an walinufaika zaidi wa mazuwaru (watu) laki moja na elfu themanini (180,000), kutokana na juhudi za Maustadhi waliokua wanafundisha katika vituo hivyo, tunatarajia kuona miaka ya mbele idadi inaongezeka zaidi, ukizingatia kua mradi huu ni miongoni mwa miradi muhimu zaidi inayo simamiwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unao husu sekta ya Qur’an, pia wana miradi mingi inayo lenga kupanua wigo wa Qur’an tukufu, ikiwa ni pamoja na kufanya mahafali, nadwa na mashindano ya Qur’an tukufu”.

Hafla ilipambwa na onyesho la filamu inayo elezea umuhimu wa harakati za Maahadi ya Qur’an tukufu, na kulikua na usomwaji wa mashairi, na mwisho kabisa Maustadhi wakakabidhiwa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: