Kamati ya misaada iliyo chini ya ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani, yatoa misaada kwa wakimbizi wa Qaaim na yasisitiza kua itaendelea na kazi yake hadi atakapo rudi nyumbani mkimbizi wa mwisho…

Maoni katika picha
Pamoja na kukombolewa ardhi ya Iraq kutoka katika udhibiti wa magaidi wa Daesh, na kuanza kurudi katika nyumba zao familia zilizo kimbia wakati wa vita vya ukombozi, bado kuna idadi kubwa ya wakimbizi wanao ishi katika mahema wakiwa na mazingira magumu ya maisha, miongoni mwao ni wakimbizi wa Qaaim katika mji wa Amiriyya Falufa, walio toa wito wa kusaidiwa haraka na kamati ya misaada iliyo chini ya ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani, kamati ambayo haija acha kutoa misaada tangu mwanzo kabisa wa kuanza kupatikana wakimbizi, imekua ikitoa misaada katika mikoa yote iliyokua na familia za wakimbizi.

Rais wa kamati hiyo Sayyid Shahidi Mussawi ametuambia kuhusu safari hii kua: “Baada ya kuwasili maombi ya kuhitaji msaada katika ofisi ya Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani, kamati yetu imeelekea katika hema hizo na kutoa misaada, na hili ndio jukumu letu tangu kuanza kupatikana wakimbizi, sawa iwe tulifika kutokana na wito au bila wito, tuna ratiba kamili ya muda na sehemu tunayo ifuata katika kugawa misaada, na tunaendelea na kazi yetu hadi mkimbizi wa mwisho atakapo rejea nyumbani kwake”.

Akaongeza kua: “Misaada tuliyo toa imehusisha vikapu vya vyakula (500) kila kikapu kina aina nane za vyakula, pia tumegawa nguo (2000) za watoto, kiongozi wa kamati alisimamia ugawaji huo kwa kusaidiana na kiongozi wa hema hizo”.

Sayyid Shahidi akabainisha kua: “Furaha za wakimbizi zilionekana wazi katika nyuso zao, wanaume, wanawake na watoto wote kwa ujumla wameshukuru na kumsifu Mheshimiwa Sayyid Marjaa dini mkuu, furaha zao ziliongezeka zaidi pale walipo badilisha nguo, kwa kuvua za zamani na kuvaa mpya, hisia za undugu na mapenzi zilitanda baina yao, wakasema kua jamii ya wairaq haiwezi kujitenga na kuacha undugu wao na mshikamano, kinacho fanywa na Marjaa dini mkuu kwa kutoa misaada ya kibinadamu kunaupa nguvu mshikamano wa kijamii”.

Maneno ya wakimbizi yalikua yanaonyesha mapenzi na heshima yao kwa Marjaa dini mkuu, wakionyesha kuthamini misaada inayo tolewa kwa wakimbizi na familia zenye shida katika miji iliyo kombolewa, wakamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie kila la kweri.

Kumbuka kua misafara ya kutoa misaada inayo fanywa na kamati ya misaada inaendelea kwa kufuata ratiba maalum ya muda na sehemu, sawa iwe katika heza za wakimbizi au katika miji iliyo kombolewa, kwa ajili ya kupunguza ugumu wa maisha ya familia za wakimbizi na kuwafanya wahisi kua Marjaa dini mkuu ndio kimbilio salama la wairaq wote wa tabaka zote, na kuondoa picha mbaya inayo tengenezwa na maadui.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: