Ugeni wa wasomi wa kusekula kutoka Malaysia: Chuo kikuu cha Ameed kinauzowefu unao kifanya kiwe bora kitaifa na kinapiga hatua ya kua bora kieneo na kimataifa…

Maoni katika picha
Siasa ya kua wazi mbele ya taasisi za elimu ya kisekula za ndani na nje ya Iraq, inazingatiwa kua moja ya misingi ya chuo kikuu cha Ameed, kilicho chini ya uongozi wa malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimesha pokea idadi kubwa ya wasomo wa kisekula na marais wa vyuo vikuu vya kiarabu na vya kimataifa, kwa ajili ya kuchangia uboreshaji wa kiwango cha elimu na kwendana na maendeleo yaliyopo katika sekta hii.

Ugeni kutoka Malaysia umetembelea chuo hiki wakiongozwa na Dokta Haidari Fauzi Shakraji ambaye ni rais wa jumuiya ya ushauri ya Malaysia akiongozana na jopo la walimu wa vyuo, ugeni huo ulipokelewa na rais wa uongozi wa malezi na elimu ya juu Dokta Abbasi Dida, aliongozana na wageni katika matembezi yao kwenye vitivo vilivyo chini ya chuo na akaelezea selebasi inayo tumika kufundishia, pamoja na vifaa walivyo navyo na vitengo vilivyo chini yao sambamba na kuelezea mipango ya baadae ya upanuzi wa majengo.

Mwishoni mwa matembezi yao ugeni ulionyesha kuridhishwa na kile walicho kiona katika chuo, Dokta Haidari Fauzi Shakraji alibainisha kua: “Ziara hii ni sawa na tofali za kwanza katika msingi wa makubaliano ya kuchangia maendeleo katika sekta ya elimu ya kisekula katika nchi yetu kipenzi ya Iraq, na kuchukua uzowefu wa Malaysia na kuuleta katika taasisi za kielimu za Iraq, ugeni huo ulikua na jopo la wasomi wa kisekula kutoka katika vyuo vikuu vya Malaysia ambao wanaham ya kufungua matawi hapa Iraq, kukitembelea chuo kikuu cha Ameed kulikua ndani ya ratiba, kwa ajili ya kuangalia kinacho fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya malezi na elimu ya juu, inaonekana uzowefu wao unawaweka katika nafasi ya ubora kitaifa na wanaelekea kua bora kieneo na kimataifa”.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Ameed ni moja ya taasisi muhimu za elimu zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kimefungua kitivo cha kwanza cha udaktari chenye kiwango sawa na vyuo vikuu binafsi vya udaktari, na wanafuata selimbasi ya kimataifa, kwa ajili ya kuhakikisha wanaongeza ufanisi na ubora kila baada ya muda fulani hukaribisha wasomi wa kisekula wenye uzowefu mkubwa katika sekta hii kwa ajili ya kunufaika na uzowefu wao, na kuangalia namna ya kuutumia kwa usahihi kwa ajili ya maslahi na maendeleo ya elimu yatakayo ifanya kua taasisi bora kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: