- 1- Kuzingatia mazingira na kuheshimu maelekezo ya wasimamizi.
- 2- Mshiriki azingatie anuani na kauli mbiu ya kongamano.
- 3- Ushiriki ulenge kitu kimoja katika kipengele kimoja miongoni mwa vipengele vya mashindano.
Aina za mashindano ni kama zifuatavyo:
Kwanza: Shindano la kazi bora ya kitaalamu (Kuchora – kazi za mikono), masharti yake ni:
- - Kazi zitakazo kubaliwa ni zilizo chorwa kwenye kitambaa au karatasi.
- - Isewe chini ya (sm. 40x50) na isizidi (sm. 70x100).
- - Iwe na vigezo vya kitalamu.
Pili: Shindano la picha bora za mnato (photograph), masharti yake ni:
- - Usiwe upigaji picha wa jadi (wa zamani) na utazingatiwa ubora wa picha.
- - Uhuru wa kuchagua aina ya picha (ya rangi – nyeusi na nyeupe).
Tatu: Bango lenye hati bora zaidi, masharti yake ni:
- - Liandikwe kwa mkono, sio kwa kutumia vifaa vya kielektrok kama vile kompyuta.
- - Maandishi yawe juu ya karatasi nyeupe yenye ukubwa wa (A4).
- - Kufuata kanuni za hati za kiarabu.
Izingatiwe hadithi ifuatayo kama mada ya hati: (Imamu Hassan (a.s) anasema: Sisi ni hoja ya Mwenyezi Mungu kwa watu na Fatuma (a.s) ni hoja kwetu).
Kamati ya maandalizi ilipanga mwisho wa kupokea kazi hizo kua ni (1 Jamadal-Thani 1439h), kuna kamati maalum ya watalamu itakayo zichuja na kupata washindi katika kila aina, washindi wa kwanza katika kila aina watapata zawadi ya (250,000) laki mbili na elfu hamsini dinari za Iraq.