Kamati ya maandalizi: Kongamano la Ruhu Nubuwwah ni dirisha linalo tuonyesha fikra na utamaduni wa bibi Zaharaa (a.s)…

Maoni katika picha
Rais wa kamati ya maandalizi ya kongamano la Ruhu Nubuwwah awamu ya pili, linalo simamiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kuanzia tarehe (8-9-10 Machi 2018m) sawa na mwezi (19-20-21 Jamadal-Thani 1439h) chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatuma (a.s) ni chemchem ya utume na tunda la peponi) amesema kua, kongamano hilo ni sawa na dirisha linalo tuonyesha fikra na utamaduni wa bibi Zaharaa (a.s), na kuziangazia kupitia harakati mbalimbali za kifikra na kitamaduni.

Ustadhat Bushra Jabbaar akaongeza kusema kua: “Hakika kongamano hili, litakalo fanyika katika ukumbi wa Swidiqah Twahirah ulio chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa makongamano muhimu ya wanawake yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, limekua linaendelea kua la kimataifa mwaka baada ya mwaka, mwaka jana zilishiriki nchi sita na mwaka huu zitashiriki nchi kumi ukiongeza na Iraq”.

Akabainisha kua: “Kuna ratiba maalumu ya kongamano hili iliyo jaa vitu vingi, kuanzia hafla ya ufunguzi itakayo shuhudia uwasilishwaji wa mada mbalimbali, hadi katika vikao vya mada za kitafiti ambavyo ni sehemu muhimu sana katika kongamano hili, zitakazo wasilishwa na watafiti kutoka ndani na nje ya Iraq, kutakua pia na visomo vya mashairi, Qur’an pamoja na maonyesho ya kazi za mikono, kama vile picha za kuchorwa na hati za kiarabu, zitakazo shiriki katika mashindano yaliyo tangazwa.

Kumbuka kua lengo la kufanya kongamano hili ni kubainisha nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) katika sekta zote, na kuondoa pazia kuhusu mchango wake wa kielimu kupitia mada zitakazo wasilishwa, na kuonyesha nafasi yake katika elimu, na kutoa elimu kwa maktaba kuhusu utukufu wa mtu huyu na athari yake katika jamii pamoja na kuweka wazi turathi za mbora wa wanawake wa ulimwenguni (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: