Maoni katika picha
Majlisi ilikua inafanywa baada ya swala ya Isha, ilikua inafunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha unafuata muhadhara wa kidini kuhusu utukufu na sifa za pekee alizo kua nazo Ummul Banina (a.s), baada ya kumaliza muhadhara ilikua inafanyika majlisi ya matam ikiongozwa na mwimbaji maarufu Mulla Baasim Karbalai, ambaye alikua anaimba kaswida zilizo amsha hisia za mazuwari na kila aliye hudhuria, akielezea utukufu, subira na jihadi aliyo pigana bibi huyu mtukufu katika njia ya Mwenyezi Mungu, kupitia kujitolea watoto wake wanne kwenda kumnusuru Imamu Hussein (a.s).
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba ya maombolezo iliyo husisha vitu vingi, ikiwa ni pamoja na kutoa mihadhara ya dini, majlisi maalumu za maombolezo, sambamba na kupokea mawakibu (misafara) ya waombolezaji kutoka ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala, wanaokuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huu.