Atabatu Abbasiyya tukufu yatangaza azma yake ya kufanya kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina (a.s) awamu ya sita…

Nembo ya kongamano
Chini ya kauli mbiu isemayo: (Kiongozi wa waumini (a.s) ni wa mwazo kati ya waabudio na anazuhudi zaidi ya wenye zuhudi) uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza azma ya kufanya kongamano la kitamaduni Amirul Mu-uminina (a.s) awamu ya sita katika mji wa Karkal kaskazini ya India katika hauza ya Ithna-Ashariyya kuanzia tarehe (13 -18) Rajabu Aswabu (1439h) kwa ajili ya kuhuisha na kuadhimisha kuzaliwa kwa bwana wa wapwekeshaji na kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), zinatarajiwa kushiriki katika kongamano hilo Ataba tukufu za (Alawiyya, Husseiniyya na Kadhimiyya) pamoja na Atabatu Abbasiyya tukufu ambao ndio wasimamizi wakuu wa kongamano hilo.

Kwa mujibu wa maelezo ya kamati ya maandalizi ya kongamano hili, kongamano litakua na ratiba itakayo husisha vitu vingi, ikiwa ni pamoja na mada kuhusu kiongozi wa waumini (a.s), mambo yatakayo leta mafanikio kama ilivyo kua katika miaka mitano iliyo pita, mji wa (Karkal) ni miongoni mwa vituo vitakavyo tusaidia kujitanua katika miji mingine siku za mbele, kwa ajili ya kuongeza wigo wa kuwasiliana na wafuasi wote wa Ahlulbait waliopo kila upande wa India, pia kongamano hili ni sawa na daraja linalo unganisha kati yao na Ataba tukufu za Iraq.

Kamati ikaongeza kua: “Tumeandaa ratiba maalumu itakayo tumika siku za kongamano, kutakua na maonyesho ya vitabu yatakayo fanywa na Ataba tukufu za Iraq, kutakua pia na vipindi vya usomaji wa Qur’an, itakayo somwa na wasomi wa kimataifa kutoka Ataba tukufu pamoja na kutembelea Husseiniyya, Misikiti, Vituo vya mayatima pamoja na watu muhimu, kutakua na shindano la ki-itikadi ambalo washindi wake watagharamiwa kwenda kutembelea Ataba tukufu za Iraq, pamoja na ratiba za ufunguzi na ufungaji zitakazo kua na mambo mbalimbali, kama vile uwasilishwaji wa mada, usomaji wa mashairi na kaswida, pamoja na vitu vingine, kutakua na tafrija ya kupandisha bendera ya Abuladhil Abbasi (a.s) katika mji wa (Lahaldaar) umbao uko umbali wa kilo meta 205 kutoka mji wa (Karkal).

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni Amiru Mu-uminina (a.s), hufanywa kwa ajili ya kuwaadhimisha watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na kwa ajili ya kutangaza utamaduni wao na mwenendo wao wa haki na historia yao tukufu ambayo umeifundisha dunia uislamu sahihi, na kuthibitisha nafasi kubwa iliyo nayo Ataba tukufu za Iraq ya kufanya makongamano, nadwa na mikutano ndani na nje ya Iraq, kupitia vitu hivyo wamefanikiwa kufungua ushirikiano wa moja kwa moja na jamii sambamba na kusimamia mambo yanayo husu madhehebu ya haki, huku wakifafanua hatua mbalimbali zilizo pitia Ataba tukufu kiujenzi na kiuongozi, na imekua vipi ndani ya muda mfupi vinara wa uongovu na kupigiwa mfano mwema katika kila sekta.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: