Toleo la jarida la tisa miongoni mwa mausua (vitabu) vya khutuba za Ijumaa…

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha (Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat) kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa jarida la tisa lenye juzuu mbili ambazo zimekusanya khutuba za Ijumaa za mwaka (2013m) sawa na (1434 – 1435h), jarida hili ni sehebu ya kukamilisha majarida ya nyuma, na mwanzo wa safari ya kukusanya na kutoa majarida mengine chini ya uhakiki na kukamilisha vigezo vya kielimu, ili ziwe rejeo za watafiti na wanafunzi wa elimu za juu.

Rais wa kitenge cha mausua na vitabu katika kituo cha Ameed Dokta Karim Hussein Naaswih Al-Khalidi amebainisha kua: “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tulifanikiwa katoa jarida lenye juzuu mbili la khutuma za mwaka 2014m, na juzuu la kwana na la pili la khutuba za mwaka 2015m, na juzuu la kwanza na la pili la khutuba za mwaka 2016m, leo hii baada ya juhudi kubwa tumefanikiwa kukusanya khutuba za Ijumaa za mwaka 2013m, kutokana na juhudi kubwa iliyo fanywa na kikosi kazi ya kukusanya na kuhakiki lugha na vinginevyo”.

Akaongeza kusema kua: “Khutuba za Ijumaa za mwaka 2013m, zilikaua na matukio mengi makubwa, huo ndio mwaka ambao Marjaa dini mkuu alijitokeza kutatua matatizo yalilo likumba taifa, na akabainisha msimamo wake na kuelezea njia za kutatua matatizo, pamoja na mada mbalimbali za Fiqhi na Usulu zilizo hudhurishwa na makhatibu wawili Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, ambao walisherehesha na kufafanua kwa kina, jambo linalo fanya fikra zao kua msingi wa masomo na majadiliano ya kielimu kwa wanafunzi wa hauza na wanafunzi wa elimu za juu pamoja na walimu na watafiti”.

Kumbuka kua miongoni mwa mausua (vitabu) vya kielimu vinavyo tolewa na kituo cha (Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat) kilicho chini ya kitengo cha habari ya utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu ni (mausua ya khutuba za Ijumaa), chini ya uhakiki wa kielimu, ili kuzifanya kua rejeo la watafiti na wanafunzi wa elimu ya juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: