Kamati ya maandalizi ya kongamano la Ruhu Nubuwwah yatangaza kukamilisha upokeaji wa mada za kitafiti zitakazo shiriki…

Sehemu ya kongamano lililo pita
Kamati ya maandalizi ya kongamano la Ruhu Nubuwwah awamu ya pili linalo simamiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana za Atabatu Abbasiyya tukufu kuanzia tarehe (8-9-10 Machi 2018m) sawa na (19-20-21 Jamadal-Thani 1439h) chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatuma (a.s) ni chemchem ya utume na tunda la peponi) imetangaza kukamilisha upokeaji wa mada zitakazo wasilishwa katika vikao vya kongamano hili.

Wamebainisha kua; wamepokea mada (71) kutoka ndani na nje ya Iraq, na zikakabidhiwa kamati maalumu ya wataalamu kwa ajili ya kuzichuja, wamezichuja na kubakia mada (64) zilizo kamilisha vigezo na masharti ya kongamano, kisha zikachaguliwa mada (10) zilizo faulu kuwasilishwa katika vikao vya kongamano, ambapo kila siku kutakua na vikao viwili, mada hamsini na nne zilizo baki zitachapishwa katika majarida maalumu.

Kamati imesisitiza kua; awamu ya pili ya kongamano hili itapendeza kushinda awamu iliyo pita, kutokana na jinsi uwasilishaji wa mada utakavyo fanyika, pamoja na aina ya washiriki wa kongamano wa ndani ya nje ya Iraq, pia utakua ni msingi mzuri kwa makongamano yajayo, na matokeo yake chanya yatachangia kuhamasisha utafiti, jambo litakalo saidia kua na maktaba ya wanawake yenye vitabu vinavyo muelezea bibi Fatuma (a.s) vyenye uchambuzi madhubuti”.

Kamati ikafafanua kua: “Kutakua na washiriki kutoka nchi za kiarabu na kiajemi, watafiti watakao shiriki wanatoka katika nchi za: (Kuwait, Saudia, Lebanon, Oman, Iran, Uingereza, Algeria, Baharain, Sirya na Tunisia) pamoja na wenyeji Iraq watakao kua na ushiriki mkubwa kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya hapa nchini, pamoja na watafiti mbalimbali na wabobezi kuhusu bibi Fatuma Zaharaa (a.s)”.

Kumbuka kua lengo la kufanya kongamano hili ni kubainisha nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) katika sekta zote, na kuondoa pazia kuhusu mchango wake wa kielimu kupitia mada zitakazo wasilishwa, na kuonyesha nafasi yake katika elimu, na kutoa elimu kwa maktaba kuhusu utukufu wa mtu huyu na athari yake katika jamii, pamoja na kuweka wazi turathi za mbora wa wanawake wa ulimwenguni (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: