Kituo cha upigaji picha wa nakala kale na kuzitunza yaongeza hakiba ya zaidi ya nyaraka 900 ambazo historia yake inarejea katika miongo tofauti ya historia ya Iraq…

Maoni katika picha
Kituo cha upigaji picha wa nakala kale na kuzitunza kilicho chini ya idara ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imechukua jukumu la kutekeleza miradi mingi inayo wasaidia watafiti kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine inasaidia kutunza turathi na kupanua wigo wa kunufaika nazo, hivi karibuni wameanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa kupiga picha zaidi ya nyaraka 900 kutoka katika hazina ya Darul Kutub Al-Wathaaiq ya Iraq, nyaraka hizo historia yake inarejea miongo tofauti katika historia ya Iraq.

Ustadh Swalahu Mahdi Abdulwahabi mkuu wa kituo cha upigaji picha wa nakala kale na kuziwekea faharasi kilicho chini ya Ataba tukufu, alipo angea na mtandao wa Alkafeel amesema kua: “Kazi yetu haijaishia kupiga picha nakala kale na vitu muhimu jambo ambalo tumesha piga hatua kubwa na tuna hazina kubwa ya picha za aina hiyo, sasa hivi tunauzowefu wa kupiga picha nyaraka za kihistoria za Iraq, na jambo hili linazingatiwa kua utunzaji bora wa ushahidi wa mambo yaliyo tokea katika taifa hili, tumefanya makubaliano na Darul Kutub Al-Wathaiq ya Iraq kwa ajili ya kupiga picha nyaraka, na hili linatokana na makubaliano tuliyo fanya hapo awali ya kufanya kazi kwa ushirikiano baina yetu”.

Akaongeza kusema kua: “Kituo kinamiliki mtambo wa kisasa wa kupiga picha, na umekua na matokea mazuri, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu tumefanikiwa kupiga picha zaidi ya nyaraka 900 ambazo historia yake inarejea miongo tofauti ya historia ya Iraq, hatua hii ni mwanzo wa hatua zingine”.

Ustadh Swalaah akabainisha kua: “Uongozi wa Darul Kutub Al-Wathaiq ya Iraq, kutokana na walicho shuhudia na kujionea utendaji wa kazi wamekubali kutoa ushirikiano wa moja kwa moja na kituo hiki na kuhakikisha tunadumisha ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya kubadilishana uzowefu kwa faida ya kila upande, jambo hili litaimarishwa kwa kufanya warsha na nadwa za kielimu na kivitendo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: