Baada ya miaka zaidi ya (50) toka kuwekwa marumaru: Mafundi na wahandisi wa Atabatu Abbasiyya wanarudia kuweka marumaru katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Sehemu ya kazi ya uwekaji wa marumaru
Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia utekelezaji wa miradi mingi iliyo pangwa kutekelezwa ndani ya kipindi maalum kutokana na umuhimu wa kila mradi, kama vile mradi wa upanuzi wa haram, kupanua uwanja wa haram tukufu, kuweka vifuniko katika baadhi ya maeneo ya jeno la Ataba tukufu, ujenzi wa tabaka la chini (sardabu) ya kaburi tukufu, pamoja na kutengeneza na kuweka dirisha takatifu, sambamba na vitu vingine, kama vile sistim ya utiaji baridi (AC), uzimaji wa moto, utoaji wa tahadhari, mawasiliano na miradi mingine mingi nafasi haitoshi kuitaja yote, orodha hii ya miradi ya ujenzi inahitimishwa na mradi muhimu sawa na iliyo tangulia, ambao ni mradi wa kuweka marumaru katika haram tukufu, kwa mara ya mwisho iliwekwa katika miaka ya sabini karne iliyopita.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh kupitia mazungumzo aliyo fanya na mtandao wa Alkafeel ameelezea kuhusu mradi huu kua: “Mradi unatekelezwa na kitengo cha miradi ya kihandishi kwa kushirikiana na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, nao ni sehemu ya kukamilisha miradi iliyo fanywa katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), iliyo sababisha kuharibika marumaru zilizopo sasa ukiongeza na ukongwe wake, kwani zina zaidi ya miaka (50), sasa umekua mradi kamili unaotekelezwa rasmi wakati hapo mwanzo ulikua unafanywa pamoja na miradi mingine”.

Akaoneza kusema kua: “Kazi hii tumeigawa katika hatua tofauti na kila hatua moja inamaeneo maalumu, hatua ya kwanza ni eneo la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) lenye ukubwa wa mita za mraba (1000), ugawaji huu ulifanyika baada ya upembuzi yakinifu, na kwa kuteua nakshi na mapambo yanayo endana na sehemu zingine za Ataba tukufu ili ujenzi wake ufanane na kumvutia mtazamaji”.

Akabainisha kua: “Hatua ya kwanza ambayo utekelezaji wake unafanana na hatua zingine inapitia hatua mbalimbali za utekelezaji ambazo ni:

  • - Kuondoa marumaru za zamani.
  • - Kuondoa vipande vya zege ya zamani na kutengeneza iliyo haribika.
  • - Kusawazisha mipasuko ya ardhi kwa kutumia vifaa maalumu.
  • - Kuweka zege juu ya ardhi yenye ubora mkubwa na inayo saidia ukaaji mzuri wa marumaru na kuzuia majimaji na vinginevyo.
  • - Kutengeneza tabaka la chuma na kuliweka chini ya zege.
  • - Kutengeneza tabaka la chini kwa ajili ya sistim ya usambazaji wa maji, mawasiliano, tahadhari ya moto na kuliunganisha na ukumbi mtukufu wa haram kwa ajili ya kuunganishwa na sistim kuu za Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • - Kuanza kwa kazi ya kuweka marumaru kunafanyika kwa kufuata vipimo maalumu ili kuhakikisha kazi hii inafanana na uwekaji wa marumaru katika ukumbi wa haram tukufu”.

Kuhusu wasifu wa marumaru amebainisha kua: “Marumaru ni za kawaiba na nadra sana zimetengenezwa katika nchi ya Itali, zinasifa nyingi nzuri, kwanza ni za kawaida, zinarangi ya kawaida na uwezo mkubwa wa kuhimili mazingira, zina upana wa (sm 4) takriban.

Swaaigh akamalizia kwa kusema kua: “Utendaji wa kazi unaendelea vizuri kama ulivyo pangwa, kutokana na ishara hizi, mradi utakamilika kwa wakati na utaongeza orodha ya kazi nzuri zilizo fanywa na mikono ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: