Kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Ameed chaangazia matibabu ya kutumia Oksijeni chini ya msisitizo wa kimataifa…

Maoni katika picha
Matibabu ya kutumia Oksijeni yanaweza kutumika kwa kutibu magonjwa ya aina tofauti, na yanatumika katika hospitali nyingi duniani, yanaponya maradhi vizuri, kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Ameed kilicho chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kujenga uhusiano na taasisi za elimu ya kisekula za kimataifa na kujifundisha uzowefu wao, na kutafuta njia bora ya utendaji kwa kukopi uzowefu wao na kuufanyia kazi, na kuhakikisha tuna nufaika nao kinadhariyya na kivitendo, tunatumia njia mbalimbali katika kuhakikisha jambo hili, ikiwa ni pamoja na kuandaa nadwa na warsha za kielimu, nadwa iliyo fanyika leo ni moja ya mbinu hizo.

Nadwa hii imefanywa leo Juma Tano (18 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (7 Machi 2018m) katika ukumbi mkuu wa kitivo cha udaktari ndani ya chuo kikuu cha Ameed, katika nadwa hii amealikwa mwiraq aishie ugenini Dokta Mahdi Abdullahi mwalimu wa udaktari wa magonjwa ya tumbo katika chuo kikuu cha New York na mkuu wa kituo cha upasuaji katika hospitali ya New York na mtaalamu wa upasuaji wa Marekani, ametoa elimu kubwa kwa walimu wa udaktari katika nadwa hii ya kielimu iliyo pewa jina la: (Matibabu kwa kutumia Oksijeni chini ya msisitizo mkubwa na kutumiwa katika kutibu maradhi tofauti na athari yake katika tiba ya sasa).

Alielezea mambo mbalimbali kuhusu kutibu kwa kutumia Oksijeni, ambayo sio njia ngeni ya matibabu, kwa muda mrefu njia hii imekua maarufu, kwa sasa inatumika kutibu maradhi tofauti na imeonshesha mafanikio makubwa.

Mkuu wa kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Ameed Dokta Samiri Hassan Rikabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tunajitahidi kufanya nadwa hizi kwa ajili ya kuchangia ukuaji wa sekta ya matibabu hapa Iraq, na kuyafanyia kazi maendeleo yanayo patikana katika sekta hii, ikiwa ni pamoja na matibabu kwa kutumia Oksijeni ambayo huchukuliwa kua ni miongoni mwa matibabu bora kwa kuponya maradhi mbalimbali, na sisi hapa Iraq tuna haja ya kunufaika na matibabu hayo.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Ameed ni moja ya taasisi muhimu za elimu zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kimefungua kitivo cha kwanza cha udaktari chenye kiwango sawa na vyuo vikuu binafsi vya udaktari, na wanafuata selibasi ya kimataifa, kwa ajili ya kuhakikisha wanaongeza ufanisi na ubora kila baada ya muda fulani hukaribisha wasomi wa kisekula wenye uzowefu mkubwa katika sekta hii kwa ajili ya kunufaika na uzowefu wao, na kuangalia namna ya kuutumia kwa usahihi kwa ajili ya maslahi na maendeleo ya elimu yatakayo ifanya kua taasisi bora kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: