Maoni katika picha
Msimamizi mkuu wa hema hizi Ustadh Ridha Naaji Sahi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu hema hizi kua: “Hema hizi ni sehemu ya huduma za kitamaduni na mapumziko yaliyo andaliwa kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kuna mambo mengi yatakayo mjenga mtumishi kiutamaduni na kumuongezea uwelewa, pamoja na mambo mengine yatakayo mfanya ajihisi yupo katika ulimwengu mwingine”.
Akaongeza kusema kua: “Tumeunda kamati itakayo simamia hema hizo zitakazo wakusanya watumishi kutoka vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kutokana na ratiba ilivyo pangwa tumegawa kwa vikosi, kila kikosi kitachukua siku nne, tayali mambo yote ya kimkakati yamesha andaliwa, tumeanza kupokea kikosi kimoja baada ya kingine kutokana na uwezo wa hema zetu”.
Sahi akasisitiza kua: “Hema hizi ni fursa nzuri ya kutambuana kwa watumishi, wote wanafanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu sehemu tofauti, kulingana na kila mtu kitengo anacho fanyia, ni mara chache sana wao kukutana sehemu moja, kwa upande mwingine ni njia nzuri ya kujua kazi ya kila mmoja baona yao, kwani kila mmoja ataelezea majukumu yake, hivyo utapatikana uwelewa kamili wa vitengo vyote vya Ataba na kazi zinazo fanywa na kila kitengo, itamsaidia mshiriki wa hema hizi kupata picha kamili ya utendaji wa vitengo vya Ataba, miongoni mwa faida za hema hizi pia ni kuongeza elimu ya dini kupitia mihadhara ya dini na mambo ya kibinadamu na mengineyo”.
Ustadh Azhar Rikabi kiongozi wa idara ya mahusiano ya vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu na mjumbe wa kamati ya usimamizi amesema kua: “Tumesha andaa ratiba kamili ya hema hizi, ratiba hiyo inajumuisha vitu vingi, kuna mambo yanayo husu dini, kutakua na mihadhara ya Fiqhi na Aqida kwa washiriki, pia kutakua na mashindano ya kidini na kitamaduni, ambapo kutakua na maswali ya Fiqhi, Aqida, Sayansi, Historia, Jogrofia na Lugha, pamoja na masomo ya mihadhara ya maendeleo ya binadamu, sambamba na vikao vya majadiliano kuhusu hali ya taifa kwa ujumla pamoja na vipindi vya burudani, kama vile mashindano ya michezo na kutembelea maeneo mbalimbali ya Ataba tukufu na maeneo ya makumbusho.