Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu chatangaza mashindano ya picha za mnato (photography) na yatoa wito wa kushiriki…

Maoni katika picha
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza mashindano ya picha za mnato (photography) ambayo matokeo yake yatatangazwa katika kongamano la Rabiu Turathi awamu ya kwanza litakalo fanyika kuanzia tarehe (30 Machi hadi 5 Aprili 2018m) katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Masharti:

  • - Kila mshiriki anahaki ya kua na picha tatu ilimradi ziashirie turathi za kiislamu kama vile (misikiti, husseiniyya, wana chuoni, Ataba na nakala kale…).
  • - Picha iwe ya aina ya (JPEG) na ubora wa (DPI 300) isizidi ukubwa wa (mb 10) na wala isiwe chini ya (mb 5).
  • - Mshiriki anahaki ya kuondoa namba katika rangi bila kufuta au kuongeza.
  • - Inaruhusiwa picha zitakazo shiriki kua za rangi nyeupe au nyeusi.
  • - Hazita kubaliwa picha zitakazo ongezwa kitu kingine.
  • - Hazita kubaliwa picha za kuchovya au zinazo husisha maandishi au alama kama vile picha ya sahihi na vinginevyo.
  • - Isiwe imesha wahi kushiriki katika mashindano mengine.
  • - Kamati inayo simamia mashindano inahaki ya kukataa picha yeyote isiyo timiza vigezo au masharti bila kutoa sababu.
  • - Kamati inayo simamia mashindano inahaki ya kuzimiliki na kuzitumia picha hizo katika machapisho yake bila kumhusisha aliye zileta.
  • - Picha ziambatanishwe na (majina matatu, wasifu wa muhusika (sv) na namba za simu).
  • - Mwisho wa kupokea picha hizo ni (25/03/2018m).

Zawadi:

  • - Mshindi wa kwanza: (500,000) dinari laki tano za Iraq.
  • - Mshindi wa pili: (300,000) dinari laki tatu za Iraq.

Pamoja na Vidani vya kumbukumbu, pia washiriki wote ambao kazi zao zitakubaliwa watapewa vyeti vya ushiriki. Picha zitumwe kwenye anuani ya barua pepe ifuatayo: Maaref2000@gmail.com
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: