Mji wa Laknau uliopo India unazingatiwa kua moja ya miji muhimu na Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na umuhimu wake katika dini, ulikua ni mji wa tatu wenye mazingira bora ya dini baada ya miji miwili Najafu Ashrafu na Qum Muqadasah, mji huu una Husseiniyya kubwa zaidi duniani iitwayo Husseiniyya Imamu Bara, una shule na hauza za dini nyingi, pamoja na idadi kubwa ya wana chuoni, huchukuliwa kua ni kitovu cha wana chuoni wa miji yote ya India, Atabatu Abbasiyya imeonyesha namna inavyo ujali mji huo kwa kufanya kongamano la Amirul Mu-uminina (a.s) mara mbili mfululizo katika mji huo, na sasa mji huu umekua ni mlango unaopitiwa na Ataba za Iraq kuingia katika bara India, pamoja na kushiriki katika matukio mbalimbaili, hivi karibuni ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umetembelea na kushiriki majlis ya kuomboleza iliyo fanywa na watu wa mji huu, baada ya wao kutuma mwaliko katika Ataba tukufu na Ataba ikakubali mwaliko huo na kuja kushiriki pamoja nao.
Muwakilishi wa Ataba na kiongozi wa ujumbe huo Sayyid Adnaan Mussawi kutoka kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ametuambia kuhusu program hii kua: “Baada ya kuelekezwa mwaliko katika Atabatu Abbasiyya tukufu wa kwenda kuhudhuria na kushiriki katika tukio la kuadhimisha mwaka mmoja tandu kufariki kwa mzazi wa mmoja wa waumini na wapenzi wa Ahalulbait (a.s) katika mji wa Laknau, naye ni Ustadh Siraju Mahdi mmoja wa wabunge wa zamani wa mji huo, ambaye ni mtu mkubwa na muhimu huko, na hafla hii kufanyika sambamba na kumbukumbu ya kifo cha Ummul Banina (a.s), tulipewa nafasi ya kuzungumza katika halfa hiyo, iliyo fanyika katika mazaru inayo fanana na malalo ya Imamu Ali (a.s), halfa hiyo ilikua na mahudhurio makubwa ya watu wa tabaka zote, tuliwasilisha salamu za kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na watumishi wote, hali kadhalika tuliwasisitiza waendelee kushikamana zaidi na misingi madhubuti ya kiislamu, na kuimarisha misingi ya undugu na tabaka zote za watu katika jamii pamoja na kuimarisha ushirikiano baina yao, na wajiepushe na jambo lolote linalo weza kuharibu sifa nzuri ya mji huo wenye mizizi ya historia, na wamfanye Imamu Hussein (a.s) kua mwongozo wao, hakika yeye (a.s) alikua ni mtu wa watu wote”.
Akaongeza kusema kua: “Tukakabidhi zawadi ya bendera kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa Ustadh Siraji Mahdi, tukawabainishia kua bendera hii ina maana kubwa, inamaanisha ikhlasi, utekelezaji na undugu wa kweli”.
Akamalizia kwa kusema kua: “Mwitikio wao kwetu ulikua mkubwa sana hauelezeki, hali kadhalika tulitembelea baadhi ya shule na hauza za dini katika mji huo, na tukakutana na baadhi ya viongozi na watu muhimu wa mji huo, wote kwa ujumla walifurahishwa sana na ziara yetu na wakatamani irudie tena siku za mbele”.