Kwa mahudhurio na ushiriki wa kitaifa na kimataifa: Idara ya shule za Alkafeel za wasichana yafanya kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwwah awamu ya pili…

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kuhuisha kuzaliwa kwa bibi Zaharaa (a.s) na kuonyesha kushikamana naye, alasiri ya Alkhamisi ya leo tarehe (19 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (8 Machi 2018m) idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza awamu ya pili ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwwah, chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatuma (a.s) ni chemchem ya utume na tunda la peponi) vikao vya kongamano hili vinafanyika katika ukumbi mkuu wa kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s), kilicho chini ya Ataba tukufu vikiwa na ushiriki wa kitaifa na kimataifa.

Hafla ya ufunguzi wa kongamano imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu wake mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar, pamoja na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo. Baada ya kusoma Qur’an ya ufunguzi pamoja na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, alianza kwa kutoa pongezi kwa waislamu wote kwa kuzaliwa mbora wa wanawake Fatuma Zaharaa (a.s), akabainisha nafasi ya bibi Fatuma na utukufu wake ulio sababisha kua mbora wa wanawake wa duniani na kua kiigizo chema kwao na taa liangazalo, hali kadhalika akaelezea maisha yake kielimu pamoja na udogo wa umri wake, akasisitiza umuhimu wa kufuata mwenendo wake na akabainisha wazi kua kujitenga na Fatuma Zaharaa (a.s) ni sawa na kujitenga na haki na kuikurubia batili, akahitimisha ujumbe wake kwa kutangaza kufunguliwa kwa kituo cha mambo ya kifamilia kiitwacho (Kituo cha utamaduni wa kifamilia).

Baada ya ujumbe huo ikafuata program ya Qur’an tukufu iliyo endeshwa na wanafunzi wa Maahadi ya Qur’an tawi la wanawake, hali kadhalika ikaonyeshwa filamu inayo elezea harakati muhimu za kielimu na kitamaduni zinazo fanywa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana.

Kisha ukafuata ujumbe wa mtafiti Shekh Ali Tijani Samawi, akazungumzia mambo mbalimbali yaliyo tokea wakati wa uhai wa bibi Zaharaa (a.s) na matatizo aliyo kutana nayo kuanzia kufariki kwa baba yake Mtume Muhammad (s.a.w.w) hadi kufariki kwake, akabainisha kua; pamoja na matatizo yote aliyo pata lakini ameendelea kua taa liangazalo katika elimu na maarifa, anaendelea kuangazia watu wanaofuata mwenendo wake pamoja na vizingiti vilivyo wekwa ili kuzuia elimu na maarifa yake visitufikie.

Baada ya hapo mjumbe wa kamati kuu ya uongozi Sayyid Adnaan Mussawi akaburudisha masikio ya wahudhuriaji kwa kuimba kaswida ya kimashairi yenye beti zilizo elezea kuzaliwa kwa bibi mtakasifu (a.s), vilevile aliwasifu viongozi wa kituo cha Sayyidah Twahirah kwa kazi kubwa waliyo fanya hadi kufanikisha swala hili.

Mashahidi pia walikua na nafasi katika hafla hii, walikumbukwa kupitia filamu iliyo elezea msimamo na ujasiri wa familia za mashahidi katika kupambana na hali ya uyatima na kuifanya kua ni tunu kwao na kujifaharisha nayo, pia zikatolewa zawadi kwa kundi la wake na wakina mama wa mashahidi walio jitolea nafsi zao kwa ajili ya kulinda taifa hili.

Baada ya hapo wahudhuriaji wakaelekea katika ufunguzi wa maonyesho ya vitu vya kiufundi vilivyo shinda katika shindano lililo endeshwa na kamati ya maandalizi ya kongamano: (picha nzuri ya kuchora, kazi nzuri za mikono, hati nzuri, bango zuri na picha nzuri ya mnato –photography-).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: