Dokta Muhammad Tijani: Fatuma Zaharaa (a.s) hajulikani ispokua kwa wachache na hajaelezewa sana katika historia, hii ni dhulma ya historia na walio iweka…

Maoni katika picha
Mtafiti wa kiislamu Dokta Muhammad Tijani amesisitiza kua: “Hakika Zaharaa (a.s) amedhulumiwa kama alivyo dhulumiwa mme wake na baba yake Mtume (s.a.w.w), mimi nilisema katika kongamano la Imamu Ridha kua mgeni kuliko wote ni Mtume Muhammad (s.a.w.w), wala msisema kua Imamu Ridha (a.s) ni mgeni, hapa ninasema kua bibi Fatuma (a.s) pia ni mgeni katika umma huu, hajulikani ispokua kwa watu wachache, na wala historia haijamuelezea vya kutosha, hii ni dhulma ya historia na walio iandika”.

Aliyasema hayo katika hafla ya ufunguzi wa kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwwah awamu ya pili linalo simamiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana za Atabatu Abbasiyya tukufu, akaongeza kusema kua: “Kwa hakika nitalia na kuwaliza katika tukio hili tukufu kwa sababu maisha yote ya Zaharaa yalijaa shida, tabu na matatizo, hata wakati wa uhai wa baba yake aliye kua hatoki nyumbani kwake wala harudi ispokua ataanzia kwa mwanaye bibi Zaharaa na kumalizia kwa mwanae, naye kama mnavyo jua jina lake la sifa anaitwa Mama wa baba yake (Ummu Abiha), wataendelea wapenzi na wafuasi wake wa zama zote kumsalimia kwa kusema: Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake na juu ya baba yake na mme wake na wanae na siri iliyo fichika kwake”.

Akaongeza kusema kua: “Fatuma Zaharaa (a.s) ndiye aliye iambia dhulma: Habana.. kwa ujasiri, na kauli mbiu ya mwanae ilikua ni (Uwe mbali nasi udhalili), hakika alinyonya maziwa ya mama huyu aliye simama imara kuwaambia madhalimu: Hakika mmekitupa kitabu cha Mwenyezi Mungu nyuma ya migongo yenu, Zaharaa ulinganiaji wake haukua kwa ajili ya kutafuta mali au uongozi, alikua anawalingania waislamu ili washikamane na kamba ya Mwenyezi Mungu, washikamane na Qur’an tukufu, washikamane na kizazi kitakasifu, ulinganiaji wake ulikua ni wa kweli”.

Tijani akabainisha kua: “Hakika Fatuma Zaharaa (a.s) alisimama imara kuwaambia waislamu kua, enyi waislamu baba yangu ametumia uhai wake wote katika kujenga umma huu msiubomoe baada yake, haya ndio aliyokua akilingania Zaharaa (a.s)”.

Tijani akawapongeza wairaq kwa kuwashinda magaidi wa Daesh kwa kusema: “Nawapongeza wairaq kwa kuikomboa Iraq kutoka kwa madaesh, lakini nakuambieni kuweni macho bado madaesh wapo, chukueni tahadhari sana bibi Fatuma anasema: (Nakubashirieni upanga mkali na nafasi kubwa ya uadui, na matatizo enezi, na uovu wa dhalimu, anajionyesha kwenu mcha Mungu wakati anauwinda umoja wenu”.

Tijani akaendelea kusema kua: “Mimi nasema na jamii inasema na Mtume anasema: Hakika Mwenyezi Mungu anachukia kwa kuchukia kwako ewe Fatuma, hakika Mwenyezi Mungu amechukia, lini utaridhia ewe Mola? Mwenyezi Mungu ataridhia pindi atakapo ridhia Zaharaa, na lini utaridia ewe Zaharaa? Pindi umma utakapo rudi katika uongofu, kwa hiyo tunasema: tunafurahi kwa furaha zao na tunahuzunika kwa huzuni zao, ndio tumefurahika kwa tukio hili, lakini tunadumu katika huzuni, hakika alikufa akiwa katika huzuni, akiwa mdhulumiwa, natamani Mwenyezi Mungu mtukufu atuongoze na tuwe nguvu moja kwa tabaka zetu zote dhidi ya asiyekua sisi, hili ndio alilo kua akilitaka Zaharaa (a.s), nasema: Amani iwe juu yako siku uliyo zaliwa na siku uliyo pata shahada, na siku utakapo ambiwa umma wa kiislamu na binadamu wote kwa ujumla: Fumbeni macho yenu kwa sababu Fatuma anapita katika Swiraat”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuongoze na atukusanye katika undugu, kwa sababu Zaharaa (a.s) anataka waislamu waungane, enyi waislamu unganeni na mfahamu kua Fatuma mama wa baba yake (Ummu Abiha) alihifadhi Qur’an tukufu na akahifadhi hadithi za Mtume kama tujuavyo, kwa masikitiko makubwa sana hakuna hadithi zake katika vitabu vya waislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: