Atabatu Abbasiyya tukufu yazawadia familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi…

Maoni katika picha
Kutokana na kufanyia kazi wito na maelekezo ya Marjaa dini mkuu ya kuzijali na kuziangalia familia za mashahidi, na kuendeleza ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kusaidia watu hao, kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni Ruhu Nubuwwah awamu ya pili katika ratiba yao wameweka kipengele cha kuwakumbuka walio jitolea nafsi zao kwa ajili ya kubakia taifa hili tukufu, wametoa zawadi kwa familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi na wanajeshi wa serikali (wake na wakina mama wa mashahidi).

Rais wa kamati ya maandalizi Ustadhat Bushra Jabbaar ametuhadithia kua: “Hakika ratiba hii ni sehemu ndogo sana ya kurudisha shukrani kwa familia hizi zilizo jitolea wapenzi wao kwa ajili ya kulinda ardhi ya Iraq na maeneo matukufu, kutokana na utukufu wa damu zao tumeendelea kuwepo na tumefanya kongamano hili, kwa utukufu wa roho za mashahidi walio loanisha udongo wa taifa hili kwa damu zao tukufu, ni wajibu kuwakumbuka na kuzikumbuka familia zao katika kila tukio, na kukumbuka kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) ni moja ya matukio muhimu”.

Akaongeza kusema kua: “Zawadi zilihusisha wahusika wakuu wa mashahidi, kama vile mama na mke, hakika wanastahiki kupewa zawadi, wao ni watukufu, na sisi ni wadaiwa kwao kwa kuwanusuru, na ni wadaiwa kwao kwa neema ya amani ambayo imepatikana kutokana na kujitolea kwao na kujitolea kwa watoto wao damu zao takatifu, ugawaji wa zawadi ulitanguliwa na filamu iliyo onyesha subira na ushujaa alio onyesha mke wa shahidi”.

Kumbuka kua zowezi la kugawa zawadi lilisimamiwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar na mtafiti wa kiislamu Shekh Tijani pamoja na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Ataba tukufu.

Ndugu wa mashahidi walionyesha kufurahishwa kwao na huduma nzuri za kibaba zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya kwao, ambao wamedumisha mawasiliano nao, na wakatoa wito kwa serikali kuu kuzikumbuka familia hizi na kuwarahisishia mchakato wa kupata haki zao, wengi wao wanatatizo la mali, na wanahisi amani na utulivu kutokana na kujitolea kwa watoto wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: