Kwa ajili ya kuchangia katika malezi ya familia za wairaq na kupunguza matatizo ya kijamii wanayo kutana nayo, Atabatu Abbasiyya tukufu imezindua kituo kinacho husika na tamaduni za familia, yaani kitakacho saidia mambo yote ya kifamilia na kuhakikisha zinaishi kwa utulivu, kitakua kinatoa huduma kwa watu wote wa familia na kuwafatilia kwa kufuata utaratibu maalumu.
Uzinduzi huo ulitangazwa katika kongamano la kitamaduni Ruhu Nubuwwa mwaka wa pili, kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ametangaza kufunguliwa kwa kituo hicho katika ujumbe wake alio toa kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano, akausifu mradi huo na kuwaomba wasimamizi wake waongeze juhudi na kuhakikisha unafanikiwa na kupanua wigo wake.
Mtandao wa kimataifa Alkafeel umekutana na kiongozi wa kituo hicho Dokta Nidhaal Hadidi ambaye ametuhadithia kua: “Makao makuu ya kituo hiki yatakua ndani ya kutuo cha Swidiqah Twahirah cha harakati za wanawake ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kitatoa huduma kwa wairaq wote kwa ujumla na hususan watu wa Karbala, baada ya jamii kufika katika hali mbaya ya mpasuko wa kifamilia, na kwa ajili ya kuzuia tatizo la talaka linalo shika kasi siku hizi na kuongezeka migogoro ya wana ndoa na wana familia, tumeona kuna umuhimu wa kufungua kituo rasmi kitakacho husika na mambo hayo”.
Akaongeza kusema kua: “Baada ya kufanya uchunguzi wa kina tukabaini kua matatizo mengi ya kifamilia yanatokana na uwelewa mdogo, na tulipo ichunguza jamii ya wairaq tukaona kuna idadi nyingi za talaka ambazo baadhi ya familia zimefikia, kwa hiyo kazi yetu ya msingi itakua ni kuzuia tatizo kabla ya kulitibu, tumeweka mpango kazi wa kuzuia matatizo kwa kupitia kufanya nadwa (darasa mjadala) za maelekezo, kituo hiki kinakusudia kuona utulivu wa kifamilia kwa kuongeza kiwango cha uwelewa wa wanawake, kwa sababu mwanamke ndio msingi wa familia na anauwezo mkubwa wa kuiongoza familia katika amani, pia tuna kitengo maalumu cha tiba za nafsi kwa watu wenye matatizo magumu, mambo yote haya tunakusudia kuona familia zinaishi kwa amani na utulivu”.