Kwa ushiriki wa watafiti kutoka ndani na nje ya Iraq: Kuanza rasmi kwa vikao vya utafiti katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwwah mwaka wa pili…

Maoni katika picha
Vikao vya kitafiti ni moja ya vipengele muhimu katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwwah mwaka wa pili, linalo simamiwa na idara ya shule wa Alkafeel za wasichana zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatuma (a.s) ni chemchem ya Utume na tunda la peponi), vikao hivyo vimeanza asubuhi ya Ijumaa kwa kushiriki watafiti kutoka ndani na nje ya Iraq, wakiwemo watafiti watatu walioshinda katika shindano la kiutafiti lililo fanywa na kamati ya maandalizi ya kongamano hili.

Vikao hivi vinafanyika ndani ya ukumbi mkuu katika kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s), vikao vya asubuhi vinasimamiwa na Dokta Numasi Madani pamoja na Dokta Fatuma Karim Rasan, na zimewasilishwa mada za kitafiti tano ambazo ni:

  • 1- Mada isemayo: (Kulinda kwa bibi Zaharaa (a.s) mwenendo wa uimamu).

Ya mtafiti Ustadhat Shaima Yaasi Omari na Ustadhat Narjis Karim Khadhiri kutoka Iraq, na utafiti wao ulishinda nafasi ya kwanza.

  • 2- Mada isemayo: (Ulingano wa maelezo ya Qur’an na maelezo ya Fadaki) ya Ustadhat Aamaal Khalf Ali Aali-Haidari kutoka Iraq.
  • 3- Mada isemayo: (Heshima ya bibi Zaharaa (a.s) na utukufu wake.. katika hadithi za Mtume na Maimamu watakasifu) ya mtafiti Mina Ibrahim Muhammad Sheikh Ahmad kutoka Baharain, mada hiyo ilishinda nafasi ya pili.
  • 4- Mada isemayo: (Mbinu za kukinaisha katika nyenzo za kuathiri kwenye khutuba ya Fadaki ya Zaharaa (a.s).. kuangalia kilicho nyuma ya habari na kujenga maudhui) ya Dokta Yusra Muhammad kutoka Iraq.
  • 5- Mada isemayo: (Mbinu za upambanaji wa bibi Zaharaa (a.s) na athari yake katika kupambana na dhulma na madhalimu katika zama zote) ya Ustadhat Zaharaa Abbasi Hassan Hashimiy kutoka Iraq.

Harakati za kitafiti zikaendelea, ilipo fika jioni vikafunguliwa vikao vya jioni na kuongozwa na Dokta Mina Mussawi na Sayyidah Mayasi Qazwini, zikawasilishwa mada tano pia kama zifuatavyo:

  • 1- Mada isemayo: (Bibi Zaharaa (a.s) ni mfano bora kwa mwanamke wa kiislamu) ya Dokta Taghridi Haidari kutoka Lebanon.
  • 2- Mada isemayo: (Mbinu za upambanaji wa bibi Zaharaa (a.s) katika kupambana na dhulma na madhalim katika lugha na istilahi) ya Ustadhat Hindu Fadhili Abbasi Husseiniy kutoka Iraq, mada hii ilishinda nafasi ya pili, ziligongana.
  • 3- Mada isemayo: (Muhtasari wa mbinu za malezi na mahitaji ya kijamii) ya mtafiti Swidiqah Sayyid Adnaan kutoka Saudia.
  • 4- Mada isemayo: (Mtazamo wa hijabu baina ya bibi Zaharaa (a.s) na Qur’an tukufu) ya mtafiti Hasanau Abduljabaar Ali Ali Akbaru kutoka Iraq.
  • 5- Mada isemayo: (Upande wa kijamii katika uhai wa bibi Zaharaa (a.s) ya Dokta Fatuma Faalih Khafaji kutoka Iraq.

Watafiti hao walipo maliza kuwasilisha walisisitiza kua, walicho wasilisha katika kongamano hili kimefuata viwango vya kiutafiti vya kimataifa, na kwamba wamechagua mada ngeni katika uwasilishwaji pamoja na kua na vionjo vingi kutoka kwa wawasilishaji au wahudhuriaji, wakasema wanatarajia semina (vikao) vijavyo vije kukamilisha mazuri ya vikao hivi kielimu.

Kumbuka kua jumla ya tafiti zilizo wasilishwa katika kamati ya maandalizi ya kongamano zilikua (71) sabini na moja, kutoka ndani na nje ya Iraq, zote zikakabidhiwa jopo la majaji walio zipitia na kuzichuja ndipo wakapasisha tafiti (64) sitini na nne, miongoni mwa hizo tafiti tatu zikapata nafasi za juu za ushindi, na mada (10) zikachaguliwa kuwasilishwa katika kongamano hili kupitia vikao viwili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: