Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake yaendesha program ya Qur’an katika ratiba ya kongamano la Ruhu Nubuwwah…

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha program ya Qur’an tukufu katika ratiba ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwwah linalo fanyika hizi sasa.

Ustadhat Manaar Jawadi mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake ametuambia kuhusu program hii kua: “Maahadi ya Qur’an tawi la wanawake ina harakati nyingi inazo fanya ndani ya makao makuu ya Maahadi au katika matawi yake yaliyo enea mikoani, kushiriki katika makongamano ni moja ya harakati zetu, tuna pongezwa na kila anaye hudhuria program zetu, na kongamano la Ruhu Nubuwwah ni moja ya makongamano ambayo tunashiriki, kama tulivyo shiriki katika kongamano la kwanza pia tumeshiriki katika kongamano hili ambalo limekua na ushiriki mkubwa kwa kuhudhuriwa na nchi nyingi zaidi, hii ni fursa nzuri ya kuwaonyesha harakati zetu za Qur’an”.

Akaongeza kusema kua: “Tuliendesha program yetu katika sardabu ya Imamu Mussa Kaadhim (a.s) katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kukubaliana na kamati inayo simamia kongamano, katika program yetu kulikua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni: Usomaji wa Qur’an tukufu, usomaji huo ulifanyika sambamba na kukumbuka kuzaliwa kwa bibi Zaharaa (a.s), na uliwasilishwa ujumbe ulio bainisha malengo ya kuanzishwa kwa Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake, na mambo makuu yanayo fanywa na Maahadi hii ndani au nje ya mkoa mtukufu wa Karbala, na imechangia vipi kupata wasichana wasomi wa Qur’an tukufu”.

Akabainisha kua: “Katika usomaji wa Qur’an wameshiriki wakina dada nane, waliburudisha masikio ya wahudhuriaji kwa visomo murua vya kitabu cha Mwenyezi Mungu na kwa sauti nzuri, hali kadhalika kulikua na usomaji wa kaswida za kiislamu zilizo elezea utukufu wa mwenye tukio (bibi Zaharaa –a.s-) pia kulikua na ushiriki mkubwa wa wasomi wa Qur’an”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: