Sayyid Ashiqar: Fatuma Zaharaa (a.s) ni sawa na jiwe la chini katika watu wa nyumba ya Mtume (a.s) naye ni chupa ya elimu ya utume na taa mfano wa nuru ya Mwenyezi Mungu…

Maoni katika picha
Katika hafla ya kufunga kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwwah lililo simamiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatuma (a.s) ni chemchem ya utume na tunda la peponi), ambalo limekamilisha ratiba zake siku ya Juma Mosi (21 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (10 Machi 2018), ambapo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar baada ya kutoa pongezi kwa wahuduriaji na umma wa kiislamu pamoja na Marjaiyya watukufu kuhusu kuzaliwa kwa bibi mtakasifu Fatuma Zaharaa (a.s) amesema kua: “Hakika kusherehekea kuzaliwa kwa Swidiqah Twahirah Fatuma Zaharaa (a.s) kuna nafasi ya pekee katika nyoyo za waumini kutokana na nafasi yake, jambo hili hawatofautiani wanao muamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho”.

Akaongeza kusema kua: “Mtume mtukufu (s.a.w.w) anasema: (Nakuachieni vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha watu wa nyumbani kwangu, hakika viwili hivyo havita tofautiana hadi vitakapo kuja kwangu mbele ya hodhi) kutokana na kushikamana na kuifanyia kazi hadithi hii tukufu, Atabatu Abbasiyya kwa maelekezo na usimamizi wa uongoni mkuu wa Ataba tukufu imeanzisha vitengo, vituo na kufanya miradi mingi, kupitia watalamu wake, wanajitahidi kutoa elimu bora ya Qur’an, dini na mambo ya utamaduni sambamba na historia ya maimamu wa nyumba ya mtume (a.s) na ubora wao, elimu hiyo wanaitoa katika ngazi ya kitaifa na kimataifa, kongamano la kitamaduni Ruhu Nubuwwah awamu ya pili ni moja ya harakati muhimu, ukizingatia kua limeandaliwa na kusimamiwa na wakina dada walio shikamana na mafundisho ya Qur’an tukufu pamoja na kizazi cha watu wa nyumba ya Mtume (a.s)”.

Akabainisha kua: “Wameandaa kalamu na akili zao kwa ajili ya kuonyesha mwenendo wa uhai wa watukufu watu wa nyumba ambayo Mwenyezi Mungu ameitakasa, wakina dada walio soma elimu ya Mwenyezi Mungu kutoka mahala sahihi, kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) ambaye ni chupa ya elimu ya utume na taa mfano wa Nuru ya Mwenyezi Mungu, mtoto wa yule ambaye alikua ni kama baina ya mipinde miwili au karibu zaidi, na mke wa aliye wadhalilisha makafiri, mama wa Hassan na Hussein (a.s), naye ni mama wa yule ambaye alijitolea maini yake kwa ajili ya dini, na mama wa yule ambaye damu ya shingo lake iliwashinda matwaghuti, naye ni mama wa kila mpenzi wa Qur’an kuanzia wakati wa Ahmadi hadi Mahdi (a.s)”

Akaendelea kusema kua: “Natoa shukrani za dhati kwa kila aliye changia kufanikiwa kwa kongamano hili, na shukrani ziwaendee wageni wote wa kongamano kutoka ndani na nje ya Iraq na kila aliye saidia kupatikana kwa mafanikio haya”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Rehma na msamaha viwafikie mashahidi wetu, na majeruhi wetu wapone haraka, familia za mashahidi ziwe na subira, kwa utukufu wa damu zao taifa limepata neema ya amani na utulivu, hakika wana hadhi kubwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: