Mahudhurio makubwa yameshuhudiwa katika ukumbi mkuu wa kituo cha Swidiqah Twahirah kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya watafiti wa masomo ya hauza na sekula kutoka ndani na nje ya Iraq, katika kipindi hiki cha sherehe za kuzaliwa kwa Fatuma (a.s), idara ya shule za Alkafeel za wasichana zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, Alasiri ya Juma Mosi (21 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (10 Machi 2018m) wamefunga awamu ya pili ya kongamano la kitamaduni na kimatifa Ruhu Nubuwwah lililo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatuma (a.s) ni chemchem ya utume na tunda la peponi) lililo dumu siku tatu.
Hafla ya kufunga kongamano ilihudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo, halfa ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukaimbwa wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar, baada ya kutoa pongezi kwa wahudhuriaji na umma wa kiislamu pamoja na Marjaiyya watukufu kutokana na kuzaliwa kwa bibi mtakasifu Fatuma Zaharaa (a.s) akabainisha kua: “Hakika kusherehekea kuzaliwa kwa Swidiqah Twahirah Fatuma Zaharaa (a.s) kuna nafasi ya pekee katika nyoyo za waumini kutokana na nafasi yake, jambo hili hawatofautiani wanao muamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho”.
Baada yake ukafuata ujumbe wa Dokta Mishal Kaadi ambaye ni mwandishi na mshairi wa kimasihi kutoka Lebanon na mpenzi wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), ameandika vitabu vingi kuhusu watu hao, alitoa udhuru ya kuhudhuria katika kongamano hili na akawakilishwa na Dokta Taghridi Haidari katika kuwakilisha ujume wake ulio sema kua: “Hakika Fatuma Zaharaa (a.s) anatokana na nyumba ambayo dunia nzima inaitukuza na kuiheshimu, na anatokana na shule inayo jua maana ya utukufu na ushujaa ,na anatokana na nasabu tukufu, alikua mwalimu katika jamii yake, mwana lugha wa kwanza khatibu asiye fikiwa usasaha wake na mwana lugha yeyote, ni mfano wa pekee katika dunia ya wanadamu, hakika alikua mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu, uislamu na haki”.
Baada ya hapo zikatolewa zawadi kwa washindi wa shindano la utafini na shindano la kazi za kiufundi yaliyo endeshwa na kamati ya maandalizi ya kongamano hili.