Mashairi yaliyo andikwa kwa maji ya uhai yasomwa na koo za wafuasi wake kwa mapenzi makubwa ya Zaharaa (a.s)…

Sehemu ya program
Uzuri wa maneno ya kimashairi ulikua na nafasi ya pekee katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwwah la mwaka wa pili, mashairi hayakutoweka, yalikuwepo na kusomwa na washairi mahiri kutoka ndani na nje ya Iraq, waliimba kuhusu utukufu wa mbora wa wanawake wa ulimwenguni (a.s).

Vikao vya usomaji wa mashairi vilivyo fanyika katika ukumbi mkuu wa kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s), kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, vilikua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele vyake ni usomaji wa kaswida za kimashairi, kipengele hicho kilifunguliwa na mshairi Ummu Haidari Waailiy kutoka katika mkoa wa Najafu Ashrafu, na kufuatiwa na mshairi Imani Daabal kutoka Baharain, kaswida yake ilikua na anuani isemayo: (Hanna Aliyyu), kisha baada yake akafuata mshairi Fatuma Sayyid Alawiy kutoka Baharain pia, kaswida yake ilikua na anuani isemayo: (Buuhun ala Khaitwil jadilah), ikafuata kaswida ya mshairi Iitidali Durush kutoka Oman, kaswida yake ilikua na anuani isemayo: (Almajdu yushriqu fi thalathi matwaalii), akafuata mshairi Zainabu Andalib kutoka Kuwait kaswida yake ilikua inasema: (Fi maulid Zaharaa), kipengele hiki kikahitimishwa na kaswida ya Dokta Ahuud Akili kwa kaswida isemayo (Swahwatul Qadar).

Hali kadhalika vikao vivyo vilishuhudia mashairi murua yaliyo somwa na washairi wawili kutoka Baharain Imani Daabal na Fatuma Sayyid Alawiy walichanganya mahadhi baina ya fus-ha na daarij.

Baada ya hapo likafuata igizo lililo fanywa kwa ushirikiano baina ya idara ya shule za Alkafeel na idara ya malezi na elimu lililo kua na anuani isemayo: (Tumuhaati) lililo onyesha nafasi ya kazi za taasisi na matokeo hasi na chanya wakati taasisi zinapo shindana, na kutofautiana misukumo ya kufanya kazi baina ya ikhlasi ya Mwenyezi Mungu mtukufu na maumbile ya kupenda kuhudumia watu, wakabainisha misukumo binafsi na kuhisi vizuri katika mafanikio binafsi, baada ya mtiririko wa maneno wanasoma kipande cha khutuba ya fadaki ya Fatuma Zaharaa (a.s), baada ya igizo hilo ukafuata ugawaji wa zawadi kwa washairi walio shiriki katika ratiba hii.

Bibi Bushra Kinani mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hili akabainisha kua: “Tulichagua washairi wanne kutoka katika nchi nne tofauti bila kuwekemo Iraq, ambazo tulipokea kaswida zao na kuziwasilisha kwenye kamati maalumu inayo ongozwa na Sayyid Adnaan Mussawiy na baada ya kuzipasisha ndio zikaingizwa katika ratiba ya kongamano, pamoja na rekodi za mashairi”.

Naye mshairi Fatuma Sayyid Alawiy kutoka Baharain amebainisha kua: “Hakika tumefurahishwa na kongamano katika kila sekta, tafiti za kielimu zilikua nzuri na makini, maandalizi yaliyo fanyika ni ya hali ya juu kabisa, mpangilio ulikua bora zaidi, ushiriki wetu umetupa utukufu na fahari, kua kwangu hapa ni kwa wito wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ili kuja kumtumikia bibi Zaharaa (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: