Mwandishi wa falsafa mkristo Dokta Mishal Kaadi: Bora kwetu ni kujifunza kutoka kwa Fatuma Zaharaa (a.s) kwa sababu ni mtakasifu katika kila kitu…

Dokta Taghridi Haidari
Mwandishi wa falsafa Dokta Mishal Kaadi amesisitiza kua: “Bora kwetu ni kujifundisha msimamo, ufasaha, maarifa na dua kutoka kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa sababu ni mtakasifu katika kila kitu”.

Hayo yamesemwa katika ujumbe alio utuma kwenye kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwwah la mwaka wa pili, kutokana na udhuru wa kuto hudhuria mwenyewe, ujume wake ukasomwa kwa niaba yake na Dokta Taghridi Haidari, ambao ulisema kua:

Ni nani Fatuma Zaharaa (a.s)? Anatokana na nyumba ambayo walimwengu wote wanaitukuza na kuiheshimu, na anatokana na shule inayo jua maana ya utukufu na ushujaa, na anatokana na nasabu tukufu, alikua mwalimu katika jamii yake, mwana lugha wa kwanza khatibu asiye fikiwa usasaha wake na mwana lugha yeyote, ni mfano wa pekee katika dunia ya wanadamu, hakika alikua mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu, uislamu na haki.

Alikataa dhulma, akapambana kulinda siasa ya haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, akapaza sauti yake pale alipo usia azikwe usiku na jeneza lake lisihudhuriwe na wale walio kataa haki na wakamuudhi.

Sisi wakristo tunamtukuza bikra Maria aliye mpigania mwanaye Issa (a.s), lakini bibi Zaharaa (a.s) anamzidi kwa jihadi yake kwa ajili ya uislamu, katika zama ngumu miongoni mwa historia ya mwanadamu katika sekta ya dini na jamii, kila alicho fanya katika uhai wake kilikua ni cha kweli na haki tupu hadi akapewa jina la sifa (laqabu) ya msema kweli (Swidiqah).

Nguvu zake na ushujaa wake aliupata kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, akawa na uwezo mkubwa wa kusapoti ujumbe wa baba yake, alibakia na msimamo wake katika mazingira tofauti hadi katika maradhi yake, akaishi na mambo makubwa, inatuumiza vipi tusirudi katika haki au tunakua wanyonge mbele ya matatizo.

Msimamo wake uliashiria maridhiano ya kisiasa, na alitaka kuonyesha tabia ya mwanamke wa kiislamu na namna anavyo weza kuizuia nafsi yake, alizipa umuhimu mkubwa hadithi za Mtume (s.a.w.w), akatangulia mwenyewe kila sehemu, akiwa amevaa hadhi kamili ya Mtume, haiwezekani kwa mwanadamu yeyote mwenye maadili mazuri kukanusha elimu yake, maarifa yake, utukufu wake, na ukubwa wa ubora wake, kutokana na elimu na adabu zake, wanachuoni wamefanya vikao vingi wakijifunza kutokana na maneno yake na vitendo vyake.

Hivi ndio alivyo ishi mtakasifu huyu aliye onyesha utukufu wa ubinadamu hadi Mtume (s.a.w.w) akasema: Hakika yeye ni mbora wa wanawake wa ulimwenguni, ni bora kwetu tujifundishe kutokana na elimu yake na ufasaha, maarifa na dua zake, hakika yeye ni mtakasifu katika kila kitu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: