Maoni katika picha
Hafla ya ufunguzi wa mradi huu imefanyika ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi pamoja na marais wa vitengo bila kusaha kundi kubwa la mazuwaru.
Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa kwa mahadhi ya kiiraq na shekh (mzee) wa kiiraq, msomaji na hafidh Muhammad Hussein Shami.
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya kuwapongeza wahudhuriaji kwa tukio hili tukufu alibainisha kua: “Atabatu Abbasiyya inatilia umuhimu miradi mingi inayo lenga kuhudumia jamii, dini na madhehebu, na miongoni mwa miradi hiyo ni miradi inayo husu Qur’an tukufu kupitia Maahadi ya Qur’an ya Ataba tukufu, imefanya harakati nyingi ndani ya mwaka huu, na miongoni mwa harakati zake ni mradi huu tunao uzindua hapa, na leo tutamvisha taji Shekh Shami ambaye ni miongoni mwa vigogo wa Iraq na marejeo ya wasomaji wa Qur’an wa Iraq, tunamuomba Mwenyezi Mungu ampe umri mrefu aendelee kua mtumishi wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) na mtumishi wa Qur’an tukufu”.
Ukafuata ujumbe wa Maahadi ya Qur’an tukufu ulio wasilishwa na mkuu wa Maahadi hiyo Shekh Jawadi Nasrawi ambaye alibainisha kua: “Ni jambo zuri kumpongeza msomaji mkubwa wa Qur’an na kufungua mradi wa Qur’an katika siku za kusherehekea kuzaliwa kwa bibi mtakasifu Fatuma Zaharaa (a.s), hakika Atabatu Abbasiyya tukufu inatilia umuhimu mkubwa miradi ya Qur’an, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa kiongozi wa wasomaji, ambao ni wa kipekee kwa kufundisha mahadhi ya kiiraq ambayo ni mahadhi ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), yanayo itwa kwa jina la (Haafidh Khaliil Ismaiil) kiongozi wa mahadhi ya kiiraq, tulianza kuhuisha njia hii kupitia mradi huo ambao hadi sasa wamesha hitimu wanafunzi wengi, pia mahadhi hayo yamepata mwitikio mkubwa katika baadhi ya nchi tulizo fanya mahafali”.
Akasisitiza kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu inajali sana uwezo wa wairaq, hadi imeandaa kongamano maalumu kwa ajili ya jambo hilo tu, kongamano la kuonyesha vipaji na ubunifu katika kila kitu, kwa kujali hilo! leo tunatoa zawadi kwa Shekh Shami, ambaye ni fahari yetu, Ataba inampa umuhimu mkubwa kutokana na nafasi yake, hakika yeye ni kiongozi wa madrasa ya usomaji wa mahadhi ya kiiraq”.
Baada ya hapo ikafuata Qur’an tukufu iliyo somwa na Mustwafa Silawi mmoja wa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa unao endeshwa na kituo cha miradi ya Qur’an, kikafuata kisomo kilicho burudisha nyoyo za wahudhuriaji cha Ahmadi Jamali mmoja wa wanafunzi wa mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomaji hapa Iraq unao endeshwa na kituo tajwa hapo awali.
Mwishoni mwa hafla Shekh Muhammad Hussein Shami akapewa taji kwa sifa ya ( Shekh wa wasomaji wa Iraq), naye Shami akasema: “Hakika mazingira niliyo yaona Karbala katika Atabatu Abbasiyya tukufu, sijawahi kuyaona katika mji mwingine wowote hapa Iraq, nimeona katika nyoyo za vijana wao kuna mapenzi ya dhati ya Qur’an tukufu, na nifahari kubwa kwangu kupewa jina la sifa (laqabu) ya Shekh wa wasomaji, naishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na Maahadi ya Qur’an tukufu pamoja na kituo cha miradi ya Qur’an kwa jambo hili zuri na kubwa, daima naomba wapate taufiq na mafanikio katika miradi yao mitukufu”.