Kwa usanifu na mpangilio unao endana na teknolojia ya kisasa: Kitengo cha dini chazindua toghuti yake rasmi na kuungana na familia ya mtandao wa Alkafeel…

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Swidiqah Kubra Fatuma Zaharaa (a.s), kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimezindua toghuti yake rasmi, iliyo shehena kurasa nyingi na milango mbalimbali inayo waonganisha na watu wa nje, itakua moja ya njia muhimu za mawasiliano na kujibu maswali pamoja na kutoa maelekezo ya dini kwa waumini sambamba na kurusha harakati zinazo fanywa na kitengo hiki, toghuti hii imetengenezwa na kupangiliwa na idara ya intanet chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Uzinduzi wa toghuti ulihudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na wawakilishi wa kitengo cha dini na kiongozi wa idara ya intanet Ustadh Haidari Mamitha, ambaye alitoa maelezo kuhusu toghuti hiyo na mbinu za kisasa walizo tumia katika kuitengeneza na kuipangilia pamoja na kuelezea milango muhimu iliyopo katika toghuti hiyo, baada ya hapo toghuti ikaingizwa katika mtandao na kuorodheshwa katika familia ya mtandao wa kimataifa Alkafeel kwa kupitia anuani ifuatayo: https://alkafeel.net/religious/index.php?main.

Miongoni mwa milango ya toghuti hii ni:

  • 1- Habari: Katika mlango huu zitarushwa harakati zinazo fanywa na kitengo hiki ndani au nje ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 2- Machapisho: Mlango huu utakua unarusha machapisho ya kitengo hiki kwa njia ya (PDF) hivyo mtu ataweza kuyafungua na kunufaika nayo.
  • 3- Hukumu za kisheria: Mlango huu utarusha hukumu za kisheria kwa watu wanao wajibikiwa na sheria (mukalafu) kwa kufuata maoni ya Marjaa dini mkuu wa Najafu Ashrafu, utakua na hukumu nyingi.
  • 4- Fatwa: Huu ni mlango muhimu sana, katika mlango huu yatatolewa majibu ya maswali mbalimbali na fatwa kwa waumini, kwa kuandika barua pepe ya swali na kujibiwa kupitia barua pepe kwa mujibu wa fatwa za Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu.
  • 5- Picha za video: Mlango huu utarusha video za mihadhara ya dini na harakati zinazo fanywa na kitengo hiki ikiwa ni pamoja na mahafali mbalimbali.

Hali kadhalika toghuti ina kipengele cha muda na sehemu ya mawasiliano, inayo kuwezesha kuwasiliana na wasimamizi wa toghuti.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar amesema kua: “Katika siku hizu tukufu tunazo kumbuka kuzaliwa kwa bibi mtakasifu Fatuma Zaharaa (a.s), tumefanikiwa kufungua toghuti rasmi ya kitengo cha dini, na kuiingiza katika mtandao wa kimataifa Alkafeel, unao angaliwa na waumini wa dunia nzima, kwa hakika hii ni juhudi kubwa iliyo fanywa na watumishi wa kitengo cha dini kwa kushirikiana na ndugu zetu wa kitengo cha habari na utamaduni, kwa kufanya jambo hili, linafupisha safari za ndugu zetu waumini katika mambo mengi ya dini yanayo watatiza”.

Shekh Basim Aalifad-am mjumbe wa kamati ya fatwa za kidini katika kitengo cha dini amefafanua kua: “Kitengo cha dini kimeona kuna umuhimu mkubwa wa kufungua toghuti hii kutokana na ulazima wa kwenda na maendeleo ya dunia, na kurahisisha mawasiliano, leo mawasiliano ni katika mambo ya lazima, wakati mwingine mtu anaweza kushindwa kuja katika Atabatu Abbasiyya au akaogopa kuuliza baadhi ya maswali moja kwa moja, hali kadhalika toghuti hii itakua ni mimbari ya kuelezea harakati za kitengo hiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: