Kongamano la kusherehekea: Atabatu Abbasiyya tukufu yashirikiana na chuo kikuu cha Dhiqaar katika furaha yake ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Swidiqah Twahirah Zaharaa (a.s)…

Maoni katika picha
Mwaka wa saba mfululizo wa kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi mtakasifu Twahirah Fatuma Zaharaa (a.s), Atabatu Abbasiyya ikiwakilishwa na idara ya mahusiana na vyuo vikuu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Dhiqaar wamefanya kongamano la kitamaduni kwa ajili ya kuhuisha tukio hili tukufu, katika ukumbi mkuu wa chuo, na kuhudhuriwa na kundi kubwa la walimu na wanafunzi wa chuo, pamoja na ugeni ulio wakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu ukiongozwa na naibu katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Bashiri Muhammad Jaasim Rabii.

Ratiba ya kongamano iliingizwa katika harakati za mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel na kufanywa ni miongoni mwa vipengele vyake, baada ya kusomwa Qur’an tukufu ya ufunguzi na kusikiliza mwimbo wa taifa na mwimbo wa Atabatu Abbasiyya pamoja na kusoma surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu wa Iraq, ulifuata ujumbe wa rais wa chuo Dokta Riyadh Shantal ambaye alibainisha kua: “Tunafurahishwa sana kwa ushirikiano huu na Atabatu Abbasiyya tukufu, haya ni matunda yaliyo tokana na vikao mbalimbali tulivyo fanya na Ataba tukufu kutokana na sera yao ya kushirikiana na taasisi za kielimu na kimalezi kikiwemo chuo chetu, katika safari ya ushirikiano wa mambo mbalimbali ya kidini, kielimu, kitamaduni na vinginevyo, leo tunasherehekea kuzaliwa kwa bibi zaharaa (a.s), hakika amezaliwa pamoja na nuru, na Maimamu watakasifu (a.s) ni watoto wake, yeye ndiye msingi wa mwanga, tunasherehekea kuzaliwa kwake, na kujenga maendeleo pamoja na kukumbuka nukta muhimu katika dini ya uislamu, tunakumbuka nafasi ya mwanamke mwenye msimamo aliye jitolea kwa ajili ya ndugu yake, tunakumbuka historia ya amani, kukumbuka huku kuwe kwetu ni msingi wa maendeleo ya taifa letu kwa wanafunzi wote wa kiume na wakike”.

Akaongeza kusema kua: “Kufungua milango ya ushirikiano na vyuo vikuu pamoja na taasisi za kielimu kuliko fanywa na Ataba, ikwemo Atabatu Abbasiyya tukufu toka mwaka (2003), ni jambo zuri sana linalo ashiria uwajibikaji wa taasisi za dini katika kuhudumia jamii, na kwamba taasisi za dini zinafanya juhudi ya kuhakikisha jamii zinapata maendeleo mazuri, tunaipongeza Atabatu Abbasiyya kwa hatua hii”.

Kisha ukafuatia ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na naibu katibu mkuu Muhandisi Bashiri Muhammad Jaasim Rabii, alianza kwa kutoa mkono wa pongezi kwa kuzaliwa mbora wa wanawake wa ulimwenguni Fatuma Zaharaa (a.s), akabainisha utukufu wa kufanya mkusanyiko huu kila mwaka, hakika mkusanyiko huu umepamba sehemu hii kwa kusherehekea kuzaliwa kwa Zaharaa (a.s), lakini jambo bora zaidi ni kuzipamba roho zetu kwa kumkumbuka, akasema: “Mwenyezi Mungu mtukufu humneemesha mja wake neema za kushikika (madiyyah) au kufikirika (maanawiyyah), neema za kushikika (madiyyah) ni kama vile kupewa riziki ya mali ambayo hubakia na dunia na huondoka kwa kuondoka kwake, mwanadamu huisha na kuondoka, amma neema ya kufikirika (maanawiyyah) neema hiyo huendelea kua pamoja nayo hata baada ya kufa kwake, neema hiyo humfaa kaburini kwake hadi siku ya kiyama, kama mwanga wa jua na mwezi vinavyo waongoza watu kuona njia, na nyota pia zinawaongoza watu bara na baharini, Mwenyezi Mungu ameweka miongozo kwa mfumo huo, itakapo kua kuna mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kama vile dini ya kiislamu na kuwatawalisha Ahlulbait, kuwepo kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake, uwepo za Zaharaa ambaye leo tunakumbuka kuzaliwa kwake hizi zote ni neema za kufikirika (maanawiyyah)”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika uwepo wa Zaharaa (a.s) ni uwepo wa kimanayiyyah, nuru yake inapo ingia katika moyo, moyo hupata rehma na huhisi kuingiwa na nuru ya Mwenyezi Mungu ndani ya moyo wa mwanadamu huyo, hii ni neema ya kweli, nuru ya Zaharaa inapoingia katika moyo wa mwanadamu, moyo hupata uongofu, (moyo bora ni wenye kujitambua) vipi moyo utajitambua? Utajitambua kwa kuwapenda Ahlulbait na kuwakumbuka, kumkumbuka Zaharaa ni mfano mkubwa wa jambo hilo, kwa kumkumbuka na kumpenda moyo unakua umejitambua, na unapo jaa imani na ukampenda Zaharaa na watoto wake utapata usaidizi wa Mwenyezi Mungu”.

Akaendela kusema: “Zaharaa (a.s) ana nafasi kubwa, Mtume (s.a.w.w) amezungumza sehemu nyingi akibainisha utukufu na nafasi ya Zaharaa (a.s), pomoja na yote aliyo sema Mtume kuhusu utukufu wake lakini bado yalimfika yaliyo mfika katika maisha yake mafupi, alifikwa na matatizo makubwa, akauawa kwa kutenzwa nguvu na akafa akiwa na huzuni, hadi akaamua kumuhusia mtoto wa ammi yake na mume wake Ali (Ewe mtoto wa ammi! Nikifa nizike kwa siri na sio kwa wazi, usiku na sio mchana) kwa nini alihusia hivyo? Ili autangazie umma kudhulumiwa kwake”.

Akamaliza kwa kusema: “Yapasa uakisi uhai wa Zaharaa (a.s) na vitendo vyake pamoja na kauli zake katika maisha yetu, yatulazimu kumuiga na kufuata mwenendo wake, tunatakiwa kumpenda na kumkumbuka pamoja na kufanya vitendo vizuri, yatupasa tunufaike na vitendo vyake kadri tuwezavyo”.

Kisha likafuata shairi lililo somwa na Ustadh Ali Hussein Zaidi, na mada ya kitafiti iliyo wasilishwa na dokta Adnaan Maalih iliyo elezea (Fatuma Zaharaa katika mapokeo ya historia tukufu), kisha yakafuata mashairi, kutoka kwa mshairi Haidari Khashaan na lingine kutoka kwa Hassan Zarkani, baada ya hapo wakapewa zawadi washindi wa shindano la Fatuma Zaharaa (a.s).

Kongamano lilihusisha vitu vingi vilivyo onyesha nafasi ya Swidigah Twahirah (a.s), sambamba na kufanya maonyesho ya vitabu, mabango ma picha za mnato (photography) zinazo onyesha historia ya mji mtukufu wa Karbala tangu kuanzishwa kwake, kisha wakagawa vidani na vyeti kwa washiriki wa kongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: