Chuo kikuu cha Ameed chafanya nadwa ya kielimu kuhusu kutibu kwa kutumia upandikizaji wa vipande…

Maoni katika picha
Miongoni mwa kuonyesha namna chuo kikuu cha Ameed kilicho chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinavyo jali mambo ya afya kwa ujumla, na kukamilisha kwa mtiririko wa nadwa zake za kielimu, kitivo cha udaktari kinaendesha nadwa ya kielimu, inayo zungumzia mtazamo muhimu kielimu na kimatibabu wa kutibu kwa kutumia upandikizaji wa vipande, yenye anuani isemayo: (Kutumia upandikizaji wa vipande ni jambo la kipuuzi au kielimu), katika ukumbi mkuu na kuhudhuriwa na jopo kubwa la wakufunzi wa chuo, wakiongozwa na mkuu wa chuo Dokta Jaasim Muhammad Marzuki pamoja na idadi kubwa ya wanafunzi.

Mada iliyo wasilishwa na Dokta Amiri Nuri Jalukhaan mbobezi wa kutibu kwa kutumia vipanbe iligusa mambo mengi, muhimu zaidi alisema: Hakika kutibu kwa upandikizaji wa vipande ni elimu inayo jitegemea japo kua haitumiki sana, pia kuna watu wengi duniani wanao tegemea zaidi tiba asili ikiwemo aina hii ya matibabu, kutokana na faida zinazo patikana katika tiba hizo. Akabainisha kua upandikizaji wa vipande ni mtazamo wa zamani una zaidi ya miaka elfu tano, miaka ya hivi karibuni njia hiyo imeboreshwa zaidi kwa kuongezwa vitu vingi na kutumia vipande vya kichina, pamoja na tafsiri za kielimu zinazo elezea mazingira ya kutumia vipande katika matibabu, bamoja na kuainisha sehemu za viungo vya mwili zinazo faa kupandikizwa vipande hivyo.

Naye Dokta Jaasim Marzuki rais wa chuo kikuu cha Ameed amebainisha kua: “Hakika nadwa hii ni miongoni mwa harakati za chuo zinazo lenga kuinua kiwango cha elimu, na kuimarisha uwelewa wa wanafunzi kwa kuwajulisha kila kitu katika ulimwengu wa tiba, ikiwa ni pamoja na kuwaelezea teknolojia ya mwisho kuingia katika sekta ya tiba kama vile teknolojia hii ya kutibu kwa kupandikiza vipande ambayo imeanza kutumika zaidi hivi karibuni, jambo linalo sababisha kua na umuhimu wa kujadiliwa na kuangalia faida zake”.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Ameed ni moja ya taasisi muhimu za elimu zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kimefungua kitivo cha kwanza cha udaktari chenye kiwango cha vyuo vikuu binafsi vya udaktari, na kinafuata selibasi ya kimataifa, kwa ajili ya kuhakikisha kinatoa elimu nzuri na kufikia katika kilele cha ubora, kila baada ya muda fulani hukaribisha wasomi na wabobezi wa kisekula kwa ajili ya kunufaika na uzowefu wao na kuangalia namna ya kuutumia kwa faida, ili kuongeza kiwango cha elimu na kukifanya kichuane na taasisi kubwa za kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: