Rais wa ofisi ya ukaguzi wa mali: Tulicho shuhudia katika miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinatupa fahari na kuonyesha uzowefu wenye mafanikio katika kusaidia uchumi na viwanda vya kitaifa…

Sehemu ya ziara
Rais wa ofisi ya ukaguzi wa mali kutoka baraza la mawaziri la Iraq, Dokta Swalahu Nuri Khalf amesisitiza kua: “Tulicho shuhudia katika miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatupa fahari kwa kua ni viwanda vya kitaifa vinavyo tegemea uwezo na uzowefu wa raia wa Iraq, ni jambo zuri lenye mafanikio katika kusaidia uchumi wa viwanda vya kitaifa”.

Aliyasema hayo baada ya kutembelea miradi kadhaa ya Atabatu Abbasiyya tukufu yeye pamoja na jopo lake, wakiongozwa na katibu mkuu wa Ataba Muhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi, Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh pamoja na jopo la viongozi.

Dokta Swalahu aliongeza kusema kua: “Kwa nafasi yetu kama ofisi ya ukaguzi wa mali ya baraza la mawaziri, tutawasilisha hali tuliyo shuhudia na tutaongea na wizara ya viwanda na madini pamoja na wizara zingine kwa ajili ya kujenga ushirikiano na kubadilishana uzowefu, kwa ajili ya kuchangia uchumi wa Iraq na kuimarisha viwanda ambavyo vina nafasi kubwa ya kukuza uchumi wa taifa”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu tangu alipo anza kuingia katika sekta ya viwanda na sekta ya afya pamoja na sekta zingine, imepiga hatua kubwa sana, imefanikiwa kusambaza bidhaa zake katika mikoa yote ya Iraq”.

Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu amesema kua: “Hakika hii ni moja ya ziara zinazo fanywa na viongozi wa serikali na wasio kua wa serikali, kwa ajili ya kuja kuangalia maendeleo ya miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, yanayo hutegemea uwezo na uzowefu wa raia wa Iraq, hii ndio sera yetu tangu mradi wa kwanza kabisa, tunataka kuujulisha ulimwengu kua wananchi wa Iraq wana akili na uwezo wa kufikiria, kubuni na kutengeneza mradi wowote na kwa kiwango chochote iwapo watapatiwa vifaa na ufadhili stahiki, hili tumeliona katika miradi yote inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na kwa upande mwingine tunatoa ujumbe kwa taasisi za serikali kua miradi ya Ataba tukufu ipo kwa ajili ya kusaidia kukuza viwanda vya Iraq na uchumi wa Iraq na sio kutoa upinzani kwa serikali”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: