Mfuasi kapambana na ulemavu wake kwa kutengeneza bango kwa meno yake na kulitoa zawadi katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Mapenzi yana sura nyingi, mtu anaweza kuonyesha mapenzi kwa anaye mpenda kwa kutumia njia tofauti, baadhi ya njia hizo ni kuonyesha hisia, kutoa zawadi na kujitolea, na njia nyingine ni kutumia uwezo wako binafsi na kutengeneza kitu cha kumpa unaye mpenda.. hili ndio lililo fanywa na Mahdiyya Baaqir kutoka Tehran nchini Iran, ulemavu wake ambao ni kupooza kwa viungo, haukumzuia kutengeneza kitu japo kidogo na kukitoa zawadi kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi hiyo hakuitengeneza kwa mikono yake wala hakukubali kusaidiwa na familia yake, bali ameifanya mwenyewe na kuimaliza ndani ya muda mfupi sana kwa kutumia meno yake.

Mzazi wake amesema kua: “Hakika Mahdiyya anatatizo la kupooza sehemu kubwa ya viungo vya mwili wake, hawezi kusikia na kuongea, alikusudia kumaliza kazi hii ndani ya siku kumi, baada ya kufahamu kua atakwenda ziara katika mji mtukufu wa Karbala”.

Kazi yenyewe ni ubao alio uchora kwa kutumia rangi mbalimbali na kuandika jina la Abulfadhil Abbasi (a.s) katikati ya ubao huo, linalo someka (Yaa Abbasi), kupitia ubao huo kaonyesha mapenzi yake kwa mwezi wa bani Hashim (a.s).. ili autoe zawadi atakapo wasili Karbala kwa kitengo cha zawadi na nadhiri cha Atabatu Abbasiyya tukufu na kuingizwa katika orodha ya vitu vinavyo pokelewa na kitengo hicho kutoka kwa wafuasi wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kila pembe ya dunia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: