Atabatu Abbasiyya tukufu yapata shahada ya kua msimamizi wa nje wa kisekula katika nchi za Falme za Kiarabu.

Maoni katika picha
Mkutano wa umoja wa vyuo vikuu vya kiarabu umemalizika katika mji wa Dubai tarehe (14 Machi 2018m) huku ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu unao ongozwa na Ustadh (Jawaad Kaadhim Hasanawi) mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya, na Dokta (Abbasi Dida) rais wa kitengo cha malezi na elimu cha Ataba tukufu, na Dokta (Mushtaqu Ali) makamo wa kitengo cha malezi, na Dokta (Jasim Ibrahimi) makomo wa mambo ya utawala, wakitunukiwa shahada ya kua wasimamizi wa nje wa masomo ya kisekula katika Falme za Kiarabu baada ya kushiriki kwao katika semina ya kujenga uwezo iliyo fanywa katika chuo cha Daru Jamiiyyah Dubai.

Tambua kua washiriki hao waliwasilisha ripoti iliyo onyesha maendeleo ya kisekula na wakapongeza wasimamizi wa semina hiyo.

Semina hiyo iliongozwa na walimu walio bobea kutoka katika nchi za kiarabu, kama vile: Oman, Misri, Lebanon, Jodan, Somalia, Falme za Kiarabu (Imaraat) pamoja na Iraq.

Ushiriki huu unafasiri muelekeo wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kukuza uwezo wake kiufundi, kihandisi na kiutumishi kwa kushirikiana na kila rafiki wa Ataba tukufu kutoka kila sehemu ya dunia, kwa sababu Ataba tukufu inataka kufikia lengo lake la kua chombo cha kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: