Allamah Profesa Hassan Issa Hakiim: Tuna haja ya kufanya uchunguzi wa turathi unaoweza kutufikisha katika ukweli…

Maoni katika picha
Katika hafla ya ufunguzi wa kongamano la kimataifa kuhusu uhuishaji katika kutengeneza historia na kuiandika linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na taasisi ya Bahrul-Uluum Al-Khairiyya, chini ya kauli mbiu isemayo (Hauza ni kitovu cha mabadiliko) lililo anza siku ya Alkhamisi (26 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (15 Machi 2018m) kulikua na ujumbe kutoka kwa Allamah Profesa Hassan Issa Hakiim, miongoni mwa aliyo sema ni: “Leo historia sio riwaya tena, bali ni elimu inayo fafanua mazingira halisi, kwa sababu tuna urithi mgumu wa riwaya zilizo changanyika nzuri na mbovu, imekua vigumu kwetu kuzichambua, hivyo inatulazimu tusome historia kielimu na kifalsafa ili tupate ukweli”.

Akaongeza kusema kua: “Wabaya wetu ni wengi, ambao kazi yao kubwa ni kukosoa yaliyomo katika vitabu vyetu, kwa sababu hatuja vichuja na kuchambua ukweli kuuweka mahala pake, hili ndilo tatizo, historia ya Mtume Mtukufu imetolewa kasoro nyingi hali kadhalika historia za maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s), kupitia kongamano hili unaweza kua mwanzo wa kuingiza historia katika hauza kama somo la falsafa, inatosha kujitenga na historia, inalazimika tuifanye kama somo la Fiqhi na Usulu, khatibu anahitaji historia kamili na anatakiwa azungumze historia chanya”.

Akasema kua: “Tunapo kutana na tatizo yatupasa kulitatua, hiki ndio kinacho takiwa katika kutengeneza historia kupitia utafiti wa maandishi na kilicho chapwa, na kuangalia mashairi na vielelezo vingine kisha kuchukua yenye manufaa nasi, na huu ndio ujumbe wa leo, hivyo tuna haja ya kuchuja taarifa, uchujaji wa turathi ndio utakao tusaidia kupata ukweli”.

Akabainisha kua: “Kuna maelfu ya nakala kale katika mahandaki (sardabu) hadi lini zitabaki huko? Lini zitahakikiwa? Kwa nini haziundwi jumuiya kwa ajili ya kuzihakiki?! Mabwana! Tunamiliki mali na akili, kwa nini tupoteze utajiri huu? Hatuoni uchungu watu walitumia umri wao kuandika vitabu, kisha vitabu vyao viishie katika mahandaki? Wala hatujui lini vitakusanywa, lini vitachomwa, lini…, tulishuhudia matukio ya mwaka (1991m) na tulishuhudia matukio mengine, nakala kale ngapi zilichomwa”.

Akamaliza kwa kusema: “Natoa wito kwa wenye mamlaka waunde kamati ya wasomi wa hauza, wa vyuo vikuu na wanatamaduni, ili watowe turathi hizi na kuzileta katika ulimwengu wa uwepo, kuna masomo muhimu sana ambayo hatuja yafikia ndani ya turathi hizo na huu ndio ukweli, na tunatarajia wanafunzi wetu watukufu wafuate mwenendo huo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: