Sayyid Muhammad Bahrul-Uluum: Nafasi muhimu aliyo nayo Marjaa dini mkuu ya kulinda taifa hili umma huu ni wajibu kuihifadhi na kuihuisha…

Maoni katika picha
Katika hafla ya ufunguzi wa kongamano la kimataifa kuhusu kutengeneza historia na kuiandika, linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na taasisi ya Bahrul-Uluum Al-Khairiyya, chini ya kauli mbiu isemayo: (Hauza ni kitovu cha mabadiliko) lililo anza siku ya Alkhamisi (26 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (15 Machi 2018m) na litadumu kwa siku mbili, kulikua na ujumbe wa taasisi tajwa ulio wasilishwa na mkuu wa taasisi hiyo Sayyid Munahammad Bahrul-Uluum, ambaye amesema kua: “Tunawakaribisha katika mji wa kiongozi wa waumini (a.s) kwenye kikao kipya miongoni mwa mfululizo wa makongamano na nadwa zinazo andaa mazingira ya hauza za kielimu katika mji wa Najafu Ashrafu, hauza hii imetoa mamujtahidi wengi, maulamaa, watafiti, wanafalsafa na wana lugha walio jaa mashariki na magharibi ya dunia, wakifundisha mema na kuonyesha maadili ya kibinadamu na kulinda umma, kwani wapo kama alivyo kua kiongozi wao na bwana wao kiongozi wa waumini (a.s), msaidizi wa wanyonge na sauti ya umma na anaye guswa na matatizo yao na machungu yao”.

Akaongeza kusema kua: “Kubainisha historia na kuisoma pamoja na kuchambua matukio yake ni jambo muhimu sana kwa faida ya vizazi vijavyo, itawasaidia kubaini uimara na udhaifu kutokana na yaliyo fanywa na watu walio tangulia, ili waweze kujiimarisha na kuboresha mustakbali wao, umma unao soma historia mara nyingi hustaarabika na huimarika, matukio ya walio pita huwasidia wasirudi nyuma, na hunufaika na historia, wahenga wanasema (Historia hujirudia)”.

Akabainisha kua: “Wanachuoni wa hauza wa karne mbili za mwisho walifanya jukumu hili la uchambuzi wa kihistoria na kuisoma kwa jicho makini, wakaweka wazi maisha ya maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kuainisha mazingatio na masomo katika maisha yao, wakashajihisha uandishi na wakaangalia maeneo mengi ambayo hayakutazamwa na wanahistoria walio pita”.

Akaendelea kusema: “Tunacho kusudia katika kongamano hili sio tu utafiti na uchambuzi wa kielimu wa wanachuoni wa hauza na athari zao katika mazingira ya Iraq na kieneo na kutengeneza kwao historia peke yake, ni kujenga uwelewa kua sisi vilevile yatupasa kutunza taarifa zetu za sasa ili iwe rahisi kwa watakao kuja baada yetu watakao kuta jengo la taifa jipya lililo tokana na juhudi zetu, na tuweze kuwaelekeza njia sahihi na ya amani”.

Akabainisha kua: “Hakika kuhifadhi taarifa za sasa ni haki ya kila umma kuhifadhi matukio yao na historia yao, hakika nafasi muhimu aliyo nayo Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu, ya kulinda taifa hili na umma huu yapasa ihifadhiwe na tuishi chini ya anuani hiyo na ihuishwe, sasa hivi ni baada ya miaka mia moja (1918m) tangu yatokee mapinduzi katika mji wa Najafu Ashrafu yaliyo tokana na misimamo ya Marjaiyya ya kuhifadhi ardhi na umoja wa watu wa Iraq, historia imejirudia, imethibitisha kua watu walio kua waaminifu kwa Marjaiyya mwanzoni mwa karne ya ishirini, bado watoto wao wana moyo uleule wa ujasiri, uaminifu na utiifu kwa Marjaiyya kwa ajili ya kulinda ardhi ya Iraq na raia wake, pamoja na hatari kubwa ya kugawika kwa taifa na kukufurishana, kwa kua selibasi za masomo hazikutuhifadhia taarifa za watu walio pigana mwaka wa (1918m), tunaogopa na sisi tusipoteze taarifa za watu walio jitolea kila wanacho miliki katika karne ya ishirini na moja bila kutunza taarifa zao na kuzifanya kua mazingatio ya taifa yatakayo nufaisha vizazi vijavyo, hili ni jukumu la watafiti, wana historia na wanasiasa, wanatakiwa kuhifadhi taarifa hizi kwa kuangalia usahihi wa matukio bila kuweka ushabiki, jukumu hili sio dogo, lina mitihani mingi lakini lina umuhimu mkubwa sana na lazima litekelezwe kwa manufaa ya mustakbali”.

Baharul-Uluum akaendelea kusema kua: “Tuna yakini kua safari yetu ni ngumu, inahitaji juhudi za pekee kutoka kwa watafiti zetu na wana historia wetu ili tuweze kusimama imara, wala tusitoe nafasi kwa watu wengine waje kutuandikia historia yetu watakavyo, tumesha fanikiwa kutengeneza historia kwa kiwango kikubwa, tunahitaji kukamilisha mafanikio hayo kwa kutunza taarifa, ili tuvijulishe vizazi vijavyo mambo tuliyo fanya, na hilo ndio jukumu la kongamano hili la kimataifa, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuwezeshe kuifanya kazi hii kwa kuweka tofali za msingi za mradi wetu mkubwa wa kuwalea wana historia na wavumbuzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: