Kwa ushiriki wa watafiti kutoka ndani na nje ya Iraq: Vikao vya kitafiti vimeanza katika kongamano la kimataifa kuhusu kuhuisha utengenezaji wa historia na kuiandika…

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza kikao cha ufunguzi wa kongamano linalo husu utengenezaji wa historia na kuiandika, linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na taasisi ya Bahrul-Uluum Al-Khairiyya chini ya kauli mbiu isemayo: (Hauza ni kitovu cha mabadiliko), vikaanza vikao vya kitafiti kwa ushiriki wa watafiti kutoka ndani na nje ya Iraq, tafiti kuhusu mada zilizo tangazwa na kamati ya maandalizi.

Siku ya kwanza ambayo vikao vyake vimefanyika katika ukumbi wa Shekh Tusi imeshuhudia vikao vitatu vifuatavyo:

Kikao cha kwanza kiliongozwa na Sayyid Ali Hakiim, katika kikao hicho iliwasilishwa mihtasari ya mada sita, ambazo ni:

 • - Mada isemayo: (Muqawama wa Kufa dhidi ya ukoloni wa Mwingereza katika mapambano (thaurah) ya ishirini… kongamano la kufa kama mfano) ya mtafiti, Ustadh Muhammad Abdurahman Arifi kutoka Misri.
 • - Mada isemayo: (Msimamo wa wanachuoni wa hauza katika mji wa Najafu Ashrafu na jihadi yao dhidi ya ukoloni wa Mwingereza… mujahidi (mfia dini) Sayyid Muhammad Kaadhim Twabatwabai kama mfano teule) ya mtafiti, Dokta Swahibu Muhammad Hussein Naswaar kutoka Iraq.
 • - Mada isemayo: (Nafasi ya ushujaa wa wanachuoni wa hauza katika mji wa Najafu Ashrafu katika kupambana na ukoloni wa Mwingereza) ya mtafiti, Ustadhat Dina Fuadi Jawaad kutoka Iraq.
 • - Mada isemayo: (Fatwa za jihadi hutibua njama za kuvamia raia na miji) ya mtafiti, Dokta Muhammad Amiin Kuurani kutoka Lebanon.
 • - Mada isemayo: (Malalo ya Imamu Ali (a.s) na historia ya ujenzi wake) ya mtafiti, Dokta Mardhiyya Muhammad Zaadah kutoka Iran.
 • - Mada isemayo: (Wanachuoni wa hauza ni watengenezaji wa historia katika kipindi cha ukoloni wa Mwingereza) ya mtafiti, Sayyid Hashim Shibri kutoka Uingereza.

Kikao cha pili kilisimamiwa na Dokta Shekh Khalidi Tamimi, na kilikua na mihtasari ya mada nne, ambazo ni:

 • - Mada isemayo: (Mtazamo wa kisiasa wa Shekh Khurasani) ya mtafiti, Dokta Muhammad Swalehe kutoka Iran.
 • - Mada isemayo: (Uandishi wa historia na changamoto za kitamaduni kwa mujibu wa Shekh Jafari Shushtari -1230/1303-) ya mtafiti, Dokta Mahraan Ismaili na Dokta Muhammad Hussein Mandhuur kutoka Iran.
 • - Mada isemayo: (Athari ya wanachuoni wa Najafu Ashrafu katika semi za dola ya Swafawiyya … Mhakiki Karkuki kama mfano) ya mtafiti, Dokta Naufal Abdul-Amiri Al-Hamaami kutoka Iraq.
 • - Mada isemayo: (Utafiti katika barua za wanachuoni wa hauza ya Najafu Ashrafu kuhusu vita ya kikatiba ya Iran) ya mtafiti, Muhammadi Ali Jalunkar kutoka Iran.

Kikao cha mwisho cha awamu hii kilikua na mihtasari ya mada sita, ambazo ni:

 • - Mada isemayo: (Vionjo vya kihistoria kwa mujibu wa mwanafalsafa wa kiislamu Ayatu Llahi Sayyid Muhammad Taqi Al-Hakiim.. kitabu Shaair Al-Aqida kama mfano) ya mtafiti, Dokta Alaa Dini Sayyid Muhammad Taqi Al-Hakiim kutoka Iraq.
 • - Mada isemayo: (Allamah Shekh Muhammad Ridha Jafari na uhuishaji wa historia ya kiislamu) ya mtafiti, Israa Abbasi Abdu kutoka Iraq.
 • - Mada isemayo: (Sayyid Abdurazaaq Muqarram… masomo katika historia yake na harakati zake kijamii 1316-1391h /1898-1971m) ya mtafiti, Dokta Shaakir Majidi Kaadhim na Ustadh Haidari Abdurazaaq Jafari kutoka Iraq.
 • - Mada isemayo: (Majengo ya mapito katika riwaya za kihistoria kwa mujibu wa Sayyid Muhammad Bahrul-Uluum) ya mtafiti, mkufunzi msaidizi Inasi Muhammad Mahdi kutoka Iraq.
 • - Mada isemayo: (Njia za uandishi wa historia kwa mujibu wa Shekh Tusi katika kitabu chake cha Al-Amaali) ya mtafiti, Hadiyah Taqwa kutoka Iran.

Vikao hivi vya kitafiti vimetoa elimu kubwa kwa wahudhuriaji na vilikua na michango ya kielimu mingi pamoja na maswali na ufafanuzi wa kina kutoka mwa washiriki, watoa mada walijibu maswali na kutoa ufafanuzi pale ulipo hitajika.

Tunatarajia kesho siku ya Ijumaa vikao vitaendelea katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu ambapo kutakua na vikao vitatu pia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: