Kwa ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu, program za kongamano la msimu wa Karbala awamu ya tano zimeanza katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad

Maoni katika picha
Kwa mwaka wa tano mfululizo Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika wiki ya kitamaduni inayo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha kiislamu Al-Kauthar, ambayo hufanywa katika mazingira ya kiimani na watu wa Ataba mbili tukufu pamoja na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) wa Pakistan, vikao vya ufunguzi vimefanyika jioni ya siku ya Alkhamisi 15/03/2018m sawa na 26 Jamadal-Thani 1439h, na kuhudhuriwa na wanachuoni wengi pamoja na ugeni wa Ataba mbili tukufu, alihudhuria pia balozi wa Iraq nchini Pakistan na kundi kubwa la wananchi, lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na bwana Aadil Karbalai ambaye ni muadhini wa Ataba mbili, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi, halafu ukafuata ujumbe wa rais wa chuo kikuu cha Al-Kauthar Mheshimiwa Shekh Ali Muhsin Najafiy ambaye alibainisha kua:

Tunawakaribisha wageni kutoka katika Ataba mbili tukufu, pia uongozi wa Pakistani unatuma salamu zake kwa taifa hilo tukufu, tumefikiwa na nyuso zenye nuru miongoni mwa masayyid na mashekh watukufu kutoka Iraq, wamekuja kushiriki katika kongamano hili, kwa nafasi yetu tunawaomba watu wa Iraq walio pata ushindi wa kihistoria dhidi ya njama za kimataifa, ushindi ulio patikana kutokana na fatwa ya Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu, Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani, hakika ni ushindi wa ubinadamu dhidi ya unyama.

Akabainisha kua: Leo watu wa Iraq wamekua kielelezo cha ushindi dhidi ya njama mbaya, amani iwe juu yao watu wenye subira na msimamo, hakika wafuasi wa Ahlulbait (a.s) hapa Pakistan wanatatizo la harakati inayo haribu sura ya madhehebu hii ya haki, lakini tunacho kiona kwa Shia wa Iraq namna walivyo simama imara na namna wanavyo fanya subira, inatupa moyo na ujasiri, kwa kupitia mkusanyiko huu utakua ni mimbari tutakayo jifunza mazuri kutoka kwao, Pakistan inauchache wa vituo vya kidini, ni matarajio yetu kongamano hili liwe ni chachu itakayo tusaidia kunusa harufu ya baraka za Ataba tukufu.

Baada yake ukafuata ujumbe wa Ataba mbili tukufu ulio wasilishwa na Shekh Munjid Kaabi kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu, miongoni mwa aliyo sema ni:

Katika vita vya kitamaduni na kujaribu kuwatenga watu na mwenendo wa haki, kongamano hili la kipindi cha Karbala (Nasimu Karbala) liwe ni kielelezo cha wafuasi wa Ahlulbait (a.s) duniani kote, washuhudie namna gani muuliwa hutukuzwa kwa damu zake, pindi Imamu Hussein (a.s) alipo walilia watu walio kusudia kumuua yeye pamoja na familia yake kwa sababu wakifanya hivyo wataingia motoni.

Akaongeza kua: Karbala bado inatoa somo kwa watu wote namna ya kujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya dini ya kiislamu, Mwenyezi Mungu ametupa mfano wa utoaji na zuhudi zilizo fanywa na Ahlulbait (a.s), na kwa upande mwingine namna walivyo simama imara dhidi ya maadui wa dini walio kua wanapotosha uislamu sahihi, leo hii tunaona muendelezo wa mwenendo mtukufu ukifanywa na majemedari wa Iraq walio jitolea kutetea misingi ya dini na ubinadamu.

Akaongeza kusema: Hakika kongamano hili ni daraja la kufikisha mwenendo wa Imamu Hussein kwa walimwengu, na kuonyesha sura sahihi ya dini ya kiislamu na wakati huo huo kubainisha mapenzi ya Ahlulbait (a.s) waliyo nayo watu wa Iraq.

Baada ya hapo ikafuata program ya Qur’an tukufu iliyo endeshwa na mahafidh wawili kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu bwana Hussein Abduridha na Mustwafa Latwifu.. kisha watu wakaelekea katika uwanja wa chuo kikuu cha Al-Kauthar kwa ajili ya kupandisha bendera ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na baada ya hapo yakafunguliwa maonyesho ya Ataba mbili yanayo fanyika sambamba na kongamano hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: