Kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kongamano la kitamaduni la bibi Fatuma Zaharaa (a.s) mwaka wa saba, ndani ya ukumbi wa chuo kikuu cha Somar katika mkoa wa Dhiqaar kwa kushirikiana na uongozi wa chuo hicho, kongamano hilo, lililo kua na vipengele vingi linafanyika kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi huyo mtakasifu.
Hafla hiyo iliyo hudhuriwa na ujumbe kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu na jopo la wasomi wa kisekula pamoja na walimu na wanafunzi wa chuo hicho, ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ukafuatia wimbo wa taifa sanjari na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Hafla ya ufunguzi ilishuhudia uwasilishwaji wa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ulio wasilishwa na Shekh Ammaar Hilali rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, na ujubme mwingine kutoka katika uongozi wa chuo hicho ulio wasilishwa na rais wa chuo, Profesa Qassim Naaif Al-Mahyawi, ambaye alielezea utukufu na hadhi ya bibi Zaharaa (a.s), akasisitiza umuhimu wa kufuata mwenendo wake na kuufanyia kazi katika maisha ya kila siku ya nyumbani na shuleni.
Hali kadhalika hafla hiyo ilipambwa na kaswida za kimashairi zilizo elezea utukufu na sifa za mbora wa wanawake wa ulimwenguni (a.s), huku kaswida zingine zikisifu ushujaa wa Hashdi Sha’abi watukufu na jeshi la serikali kutokana na ushindi walio pata dhidi ya magaidi wa Daesh, nayo Atabatu Abbasiyya ikatoa midani kwa uongozi wa chuo kutokana na namna unavyo jali na kufanya mahafali za aina hii.
Kisha wahudhuriaji wakaelekea kwenye uzinduzi wa maonyesho ya vitabu na picha, yaliyo dhihirisha hazina iliyopo katika makumbusho ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na maonyesho mengine ambayo kilishiriki kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu.