Shirika la Aljuud pamoja na vitalu vya Alkafeel wapandisha bendera ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika program za wiki ya kilimo na siku ya mti katika uwanja wa maonyesho mjini Bagdad…

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa kushiriki maonyesho ya ndani na nje ya kitaifa na kimataifa, Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika maonyesho ya wiki ya kilimo na siku ya mti awamu ya kumi, yanayo simamiwa na wizara ya kilimo chini ya kauli mbiu isemayo: (Tuifanye Iraq kua kijani kibichi) kuanzia (14-21 Machi 2018m) katika uwanja wa maonyesho ya kimataifa Bagdad.

Wawakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu walio peperusha bendera yake katika maonyesho haya ni:

Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud

Katika maonyesho haya wamekuja na aina mbalimbali za mbolea na baadhi ya bidhaa zilizo sajiliwa kwa jina la shirika, pamoja na dawa tofauti za kutibu maradhi mbalimbali ya mimea zinazo saidia sana kuendeleza kilimo.

Ufugaji wa nyuki wa Alkafeel chini ya vitalu vya Alkafeel

Wamekuja na aina tofauti za asali, ambayo ni asili mia kwa mia, inayo zalishwa kwa kutumia njia za kisasa zinazo kubalika duniani, ikiwa ni pamoja na: asali ya Calptose, Coktel, Bressem, Matbulul pamoja na asali safi, hali kadhalika wameonyesha aina tofauti za nta, ambazo zinaweza kutumika kutibu maradhi mbalimbali sawa ime ni (Propolis) moja kwa moja au kwa kuchanganya na vitu vingine, hakika ubora wa bidhaa zetu na bei vimewafanya watumiaji wengi watuamini.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa matawi yaliyo shiriki katika maonyesho haya, ushiriki huu umetokana na maelekezo ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuchangia uzalishaji wa ndani na kuonyesha mafanikio na kuyaelezea, kwa upande mwingine ushiriki huu ni njia muhimu ya kuwasiliana na ulimwengu wa nje na kuangalia maendeleo yaliyopo katika sekta husika.

Ustadh Maitham Bahadeli kiongozi mtendaji wa shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud, amesisitiza kua lengo kuu la kushiriki katika maonyesho haya, ni kufikisha ujumbe wa wazi kua Iraq inawatu wenye uwezo mkubwa, wanaweza kuleta ushindani wa kiviwanda, na inaweza kuimarisha uchumi wake iwapo itapewa fursa na kuwezeshwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: