Hospitali ya rufaa Alkafeel yashiriki katika maonyesho ya huduma za afya, na waziri wa afya asifu ushiriki huo…

Maoni katika picha
Waziri wa afya na mazingira Dokta Adila Hamud ameisifu hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na huduma za matibabu inazo toa kwa wananchi wa Iraq, tena kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa zaidi na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya Iraq, jambo ambalo limekua na matokeo chanya katika sekta ya afya kutokana na huduma zao zinazo chuana na hospitali za kimataifa, akaomba hospitali iendelee kutoa huduma na kuboresha zaidi utendaji wake.

Aliyasema hayo alipo tembelea tawi la hospitali ya Alkafeel linalo shiriki katika maonyesho na kongamano la wahudumu wa afya linalo endelea hivi sasa katika uwanja wa maonyesho ya kimataifa wa Bagdad (HIME).

Ushiriki wa hospitali hiyo kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa hospitali Dokta Haidari Bahadeli: “Yanafanyika kwa ajili ya kuangalia mbinu mpya zaidi katika kutoa huduma za kimatibabu zinazo fanywa na hospitali za kitaifa na kimataifa, na kuangalia matokeo ya dawa zinazo tumika katika matibabu na zinazo faa kutumiwa mahospitalini, kwa upande mwingine, kuzitambua taasisi zinazo toa huduma za tiba ambazo zimeanza kua za kimataifa hata kama zina muda mfupi tangu zisajiliwe ukilinganisha na baadhi ya hospitali kubwa, tawi letu katika maonyesho haya, linaonyesha mafanikio yaliyo patikana ndani ya miaka miwili katika kutoa huduma kwa raia na kutibu maradhi, na aina mbalimbali za upasuaji zilizo fanywa na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya Iraq, pamoja na mchango wake katika kutibu majeruhi wa jeshi la serikali na wale wa Hashdi Sha’abi, na huduma za bure ulizo tolewa kwa makundi mbalimbali ya jamii”.

Kiongozi wa tawi la hospitali Ustadh Hassan Aaridhi aliongeza kusema kua: “Tawi la hospitali limepata mwitikio mkubwa sana kutoka kwa watu wanaokuja kutembelea maonyesho haya, wanaonyesha kushangazwa na ubora wa huduma zinazo tolewa na ambazo hazipatikani katika baadhi ya hospitali za Iraq, tumekua tukielezea huduma zetu pamoja na kujibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi, hakika maonyesho yamekua na mafanikio makubwa, tumeweza kuelezea mafanikio yaliyo patikana katika hospitali kwa kila aliye kuja kututembelea na kwa viongozi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: