Kuhitimisha vikao vya utafiti katika kongamano la kuhuisha utengenezaji wa historia na kuiandika…

Maoni katika picha
Baada ya siku mbili za harakati za kielimu kutoka kwa watafiti wa kihauza na kisekula wa ndani na nje ya Iraq, ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Ijumaa ya tarehe: (27 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (16 Macha 2018m) ulishuhudia kikao cha kuhitimisha kongamano la kimataifa kuhusu kuhuisha utengenezaji wa historia na kuiandika, lililo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Hauza ni kitovu cha mabadiliko), linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na taasisi ya Bahrul-Uluum Al-Khairiyya.

Vikao vya mada za kitafiti vya siku ya pili vilikua vitatu, ambavyo ni muendelezo wa vikao vilivyo tangulia, kikao cha kwanza kilisimamiwa na Profesa Aadil Nadhir, na kilikua na uwasilishwaji wa mihtasari ya mada tano, ambazo ni:

 • 1- Mada isemayo: (Nafasi ya wanachuoni wa Jabal Aamir katika muamko wa kielimu wa Najafu Ashrafu kuanzia karne ya kumi hijiriyya hadi mwishoni mwa karne ya kumi na nne hijiriyya) ya mtafiti, Shekh Hassan Bagdadi Al-Aamiliy kutoka Lebanon.
 • 2- Mada isemayo: (Uhusiano wa Jabal Aamil na Iraq kwa mujibu wa riwaya za Sayyid Muhsin Amiin… masomo katika “A’yaani Shia”) ya mtafiti, Dokta Hassan Ibrahim kutoka Iraq.
 • 3- Mada isemayo: (Mtazamo wa islahi na uhuishaji katika kumbukumbu za Allamah Shekh Abdulkarim Jazaairiy) ya mtafiti, Mheshimiwa Swabihi Numani Al-Khuzaai kutoka Iraq.
 • 4- Mada isemayo: (Mfano wa mwenendo mpya katika uandishi wa historia… uchunguzi katika sharti za maudhui na njia za kuchambua historia – Taqi Hakiim kama mfano) ya mtafiti, Shekh Usama Atabi kutoka Iraq.
 • 5- Mada isemayo: (Mtazamo wa kisiasa kwa wanachuoni wa Shia Imamiyya… Shekh Abdulkarim Zanjaniy (1887-1968) kama mfano) ya mtafiti, Dokta Muhammad Jawaad Jaasim Al-Jazaairiy kutoka Iraq.

Kikao cha pili kiliongozwa na Dokta Karim Naasih Khalidi, kilikua na mihtasari mitano ya mada za kitafiti, ambazo ni:

 • 1- Mada isemayo: (Mchango wa washairi wa Najafu katika vita ya Shia na thaura ya ishirini… Ahmadi Swafi Najafiy kama mfano) ya mtafiti, Dokta Haidari Zawin kutoka Iraq.
 • 2- Mada isemayo: (Mapokezi ya kihistoria kwenye hauza ya Najafu katika kitabu cha “Al-Azhaaru Arjiyya fil Aathaari Farjiyya” cha Shekh Amraan (1398h /1978m)) ya mtafiti, Wasaam Abbasi Muhammad Sab’u kutoka Baharain.
 • 3- Mada isemayo: (Taasisi ya Kaashifu Ghitwaa na utunzaji wa kumbukumbu na kuzisambaza) ya mtafiti, Mustwafa Naajih Sifaji kutoka Iraq.
 • 4- Mada isemayo: (Amana ya elimu na uandishi wa historia) ya mtafiti, Dokta Ali Yusufu Nurdini kutoka Lebanon.
 • 5- Mada isemayo: (Fikra ya kuweka ukaribu baina ya madhehebu za kiislamu katika barua, kati ya wanachuoni wa Najafu Ashrafu na chuo kikuu cha Azhar Misri (kuangalia zaidi mitazamo ya Allamah Kaashifu Ghitwaa)) ya mtafiti, Dokta Muhammad Ali Jalunkar na Dokta Muhammad Baaqir Khuzaailiy kutoka Iran.

Kikao cha mwisho kiliongozwa na Dokta Alaa Mussawiy, kilikua na uwasilishwaji wa mihtasari ya mada tatu ambazo ni:

 • 1- Mada isemayo: (Mtazamo wa ukosoaji wa riwaya kwa mujibu wa Sayyid Abdurazaaq Muqaram) ya mtafiti, Dokta Falaah Razaaq Hashim kutoka Iraq.
 • 2- Mada isemayo: (Mtazamo wa Anthropolojia katika manhaji ya Shekh Muhammad bun Ali Hirzu Din) ya mtafiti, Ustadh Hassan Kandi kutoka Iraq.
 • 3- Mada isemayo: (Wanalugha wa hauza ya Najafu Ashrafu na vita dhidi ya ukoloni – shairi la Shekh Muhammad Ridha Shabibi kama mfano) ya mtafiti, Hussein Saaidiy na Dokta Aatwi Abayati kutoka Iran.

Vikao hivi vimetoa elimu kubwa kwa wahudhuriaji na vilikua na michango ya kielimu mingi pamoja na maswali na ufafanuzi wa kina kutoka mwa washiriki, watoa mada walijibu maswali na kutoa ufafanuzi pale ulipo hitajika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: