Hafla ya wanawake kwenye sherehe za msimu wa Karbala katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad

Maoni katika picha
Program za kongamano la msimu wa Karbala linalo simamiwa na Atabatu Husseiniyya na kushiriki Atabatu Abbasiyya, katika siku ya pili ya Ijumaa tarehe 16 Machi sawa na 27 Jamadal Thani 1439h, zilishuhudiwa hafla za wanawake zilizo andaliwa na wanafunzi wa chuo cha Al-Kauthar na kuhudhuriwa na ugeni wa Ataba mbili, katika mnasaba wa kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s), hafla hiyo ilitanguliwa na khutuba ya ukaribisho kutoka kwa wanafunzi wa chuo, ambapo walitoa shukrani kwa wageni kutoka katika Ataba mbili kwa kushiriki pamoja nao katika kongamano hilo.

Baada ya hapo Mheshimiwa Sayyid Adnaan Jalikhaan Mussawiy Imamu wa jamaa katika ukumbi wa haram tukufu ya Abbasi akazungumza, miongoni mwa aliyo sema ni:

Imetufurahisha sana kukutana na ndugu zetu wapenzi wa Ahlulbait (a.s) katika mji huu mtukufu, sisi tumekuja kutoka Karbala tumukubebeeni manukato yake katika chuo kikuu cha Al-Kauthara ambacho kimetupa mapokezi mazuri.

Akaongeza kusema kua: Katika mkusanyiko huu wa wanawake unao fanywa kwa ajili ya kusherehekea kuzaliwa kwa Fatuma Zaharaa (a.s), ingekua vizuri kwetu kama tungeifanya siku hii kua siku ya mwanamke duniani, kwa sababu kuzaliwa kwake kulileta mabadiliko ya aina yake katika jamii ya wanawake, baada ya kua mwanamke alikua anadhalilishwa na kudharauliwa, kutokana na namna Mtume alivyo kua akiamiliana naye, alikua anasimama kwa kuingia kwake na anasema anapo pata hamu ya kunusa harufu ya pepo alikua anamnusa Fatuma (a.s).

Akaendelea kusema: Kwa hakika tukiangalia haki ya mwanamke katika uislamu, utakuta kapewa haki ya kusoma, haki ya kuchagua, kapewa haki sawa na mwanaume, pamoja na hivyo mwanamke ni sawa na nusu ya jamii kutokana na umuhimu wake katika kujenga familia, kupitia malezi ya watoto hakika yeye huwapa chakula cha mwili na chakula cha roho ambacho ni kumpenda Muhammad na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Akamalizia kwa kusema: Tukiangalia katika historia tutaona wanawake walio amini ujumbe wa Mwenyezi Mungu walikua ni Asiya, Maryam na Khadijatu Kubra, amma Zaharaa (a.s) yeye alikua na nafasi ya kulinda ujumbe wa kiislamu, na kuuhami uimamu, kwa kumlinda Imamu kiongozi wa waumini asiuawe, hivyo yatupasa tujifunze subira na kujitolea katika dini, kutokana na bibi huyu mtukufu, namuomba Mwenyezi Mungu awalinde na kuwawezesha katika mambo yenye heri na dini na kila sifa njema anastahiki Mola mlezi wa walimwengu.

Baada ya hapo wanafunzi wakafanya maonyesho kuhusu tukio la kuzaliwa kwa bibi Fatuma (a.s), na mwisho wa hafla baadhi ya wanafunzi walio kua na mchango mkubwa katika kufanikisha hafla hii wakapewa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: